Tuesday, July 1, 2014

TIMU YA MBEYA CITY YAFANYA MCHAKATO WA USAJILI 2014/2015.



Kikao cha bodi kilichoketi tarehe 19/6/2014 kiliazimia kuwa klabu imefunga rasmi zoezi la usajili kwa msimu ujao wa 2014/2015. Hii ni kutokana na klabu kuwa na mipango ya kupunguza kikosi ili kuwa na kikosi kidogo na chenye ufanisi(tija) na kwa kuzingatia klabu kwa msimu uliomalizika na msimu ujao kutokuuza wachezaji wake.

Baadhi ya wachezaji watapandishwa toka katika kikosi cha pili na wachezaji wawili wapya waliojiunga na timu kwa ajili ya msimu ujao 2014/2015 wanatosha.
Mchakato unaoendelea toka tarehe 25/6/2014 ni kutafuta wachezaji kwa ajili ya kikosi cha pili (Juniour team) A na A2, mchakato huu utamalizika tarehe 2/7/2014. Lengo ni kupata wachezaji wenye umri kati ya miaka 17-21.

Wachezaji ambao muda wao wa kuendelea kuitumikia klabu umefikia tamati ni hawa wafuatao: Aziz Sibo(mkataba umekwisha muda wake 31/5/2014), Mohamed Suleiman(Kapangiwa majukumu mengine), Baraka Haule, Francis Casto, Jeremiah John Mangasini, Richard Brown, Yusuph Wilson(kutolewa kwa mkopo), Geofrey Jackson(kutolewa kwa Mkopo).

Watumishi ambao mikataba yao imekwisha muda wake na kwa sababu mbalimbali zinazojulikana kwa pande zote mbili imeshindikana kuihuisha ni Fredy Jackson aliyekuwa Afisa Habari(mkataba wake umekwisha tarehe 31/05/2014) na aliyekuwa Kocha msaidizi Maka Mwalwisi (Mkataba wake umeisha tarehe 30/06/2014).

E.E.Kimbe
KATIBU MKUU
MCC FC

0 Responses to “TIMU YA MBEYA CITY YAFANYA MCHAKATO WA USAJILI 2014/2015.”

Post a Comment

More to Read