Tuesday, July 8, 2014
UNAZIJUA NUSU FAINALI TANO ZA KIHISTORIA KATIKA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA?
Do you like this story?
fainali
ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil inaanza leo. Hapa ni nusu fainali
tano zilizochezwa na kuacha historia kubwa katika ulimwengu wa soka.
1954-HUNGARY
4 URUGUAY 2.
Hii ndio
nusu fainali inayosemwa kuwa kubwa zaidi katika michezo ya nusu fainali za
kombe la dunia. Hungary iliyoiharibu Ujerumani Magharibi kwa mabao 8-3 katika
mchezo wa makundi, iliongoza kwa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa watetezi Uruguay
mpaka dakika za mwisho na kuonekana inatinga fainali.
Lakini
taifa hilo la Amerika kusini lilipambana kupitia kwa Juan Hohlberg aliyefunga
mabao mawili na kuipeleka mechi katika dakika za nyongeza.
Mabao
mawili ya kichwa kupitia kwa Sandor Kocsic, aliyefunga mara 11 katika
mashindano yote, yaliipa Hungary ushindi wa mabao 4-2. “Ilikuwa nusu fainali
nzuri mno, ilikuwa mechi ya kasi, ufundi kwa timu zote”. Alisema nyota wa
Hungary, Jozsek Boszik. Lakini walipoteza tena kwa mabao 3-2 dhidi ya Ujerumani
Magharibi katika mechi ya fainali.
1966-
ENGLAND 2 PORTUGAL 1
Ureno
wakijivunia zaidi nyota wao mkali `Black Panther` Eusebio katika fainali
hizo walipoteza mchezo dhidi ya England. Mabao mawili ya Bobby Charlton
yaliwafanya wenyeji waongoze kwa mabao 2-0 mpaka dakika 10 za mwisho.
Eusebio,
aliyenyimwa nafasi za kufunga na kipa wa England, Gordon Banks kwa muda wote wa
mchezo, alipata penati dakika ya 83 na kufunga. Hili lilikuwa bao la kwanza kwa
England kufungwa katika mashindano hayo.
Licha ya
kupata presha katika dakika za mwisho, England walifuzu fainali. “Kile kilikuwa
kiwango kikubwa zaidi walichoonesha England mpaka leo hii,” alisema kocha Alf
Ramsey. Wakati mpinzani wake, kocha wa Ureno, Otto Gloria alisema England
itaifunga Ujerumani katika mchezo wa fainali kama itacheza soka kama lile.
Ujerumani walitegemea sana soka la nguvu”. Alisema.
1970-ITALIA
4 UJERUMANI MAGHARIBI 3
Ukikumbuka
mchezo huu wa karne ya 20, Italia walipata bao la kuongoza dakika nane tu za
mchezo kupitia kwa Roberto Boninsegne na waliamua `kupaki` basi mpaka dakika ya
mwisho ambapo Uwe Seeler alisawazisha.
Bao hilo
liliupeleka mchezo katika dakika za nyongeza. Gerd `Der Bomber` Muller
aliifungia Ujerumani bao la kuongoza, lakini Italia wakasawazisha, kabla ya
kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Luigi Riva.
Muller
alifunga tena, lakini wakati Wajerumani wakiendelea kufurahia bao hilo, Italia
walifunga bao la nne kupitia kwa Gianni Rivera na bao hilo likamaliza mchezo.
Italia walicheza mpira mkubwa dhidi ya Brazil katika mchezo wa fainali, lakini
walipoteza kwa mabao 4-1.
1980-UJERUMANI
MAGHARIBI 3 UFARANSA 3 ( UJERUMANI WALISHINDA KWA PENATI 5-4).
Ilikuwa
mechi ya maajabu. Ujerumani walifunga bao la kuongoza kupitia kwa Pierre
Littbarski. Lakini Ufaransa walisawazisha kwa penati kupitia kwa Michel
Platini. Muda wa nyongeza Ufaransa walifunga mabao mawili kupitia kwa Marius
Tresor na Alain Giresse. Hata hivyo, Ujerumani walisawazisha na kuwa 3-3
kupitia kwa Karl-Heinz Rummenigge na Klaus Fischer. Maxime Bossis alikosa
penati iliyookolewa na kipa Schumacher na Ujerumani kushinda kwa penati 5-4.
Ufaransa walikuwa wabunifu, lakini Ujerumani walikuwa na nguvu.
1998-UFARANSA
2 CROATIA 1.
Wenyeji
Ufaransa walikosolewa sana mpaka kufika hatua ya nusu fainali. Croatia
wakishiriki fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza baada kujitenga na
Yugoskavia, walifunga bao la kuongoza dakika moja tu baada ya kipindi cha pili
kuanza kupitia kwa Davor Suker. Hata hivyo, Ufaransa walisawazisha dakika moja
baadaye kupitia kwa beki wake Lilian Thuram, hilo likiwa bao lake la kwanza
katika soka la kimataifa. Thuram pia alifunga bao la pili, alipiga magoti na
kushangilia sana. Kitu pekee cha huzuni katika mechi ile ilikuwa ni kitendo cha
Slaven Bilic kupigwa kichwa na Laurent Blanc na kusababisha Blanc apate kadi
nyekundu. Alikosa mechi ya fainali ambayo Ufaransa walishinda mabao 3-0 dhidi ya
Brazil.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UNAZIJUA NUSU FAINALI TANO ZA KIHISTORIA KATIKA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA?”
Post a Comment