Monday, July 21, 2014
WALIOUA KWA DENI LA SHILINGI 9,600 WANYONGWA WILAYANI ROMBO.
Do you like this story?
WATU watatu wakazi wa Wilaya ya Rombo
mkoani Kilimanjaro wamehukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa baada ya
kupatikana na hatia ya kufanya mauaji.
Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama Kuu
Kanda ya Moshi iliyokuwa ikiendesha vikao vyake katika Mahakama ya Wilaya ya
Rombo chini ya Jaji Amaisario Munisi.
Awali kabla ya kusoma hukumu hiyo,
Mwanasheria wa Serikali, Tamari Mndeme aliwataja watuhumiwa hoa kuwa ni Plasid
Herman, Wiliadi Evaristi na Samsoni Kanje Myovela wanaokabiliwa na tuhuma za
kumuua kwa makusudi mkazi wa Kijiji cha Nayeme Tarafa ya Tarakea, Anastazia
Nicodemu.
Alisema watuhumiwa hao walitenda kosa
hilo Mei 23, 2010 katika Kijiji cha Nayeme Tarafa ya Tarakea wilayani Rombo,
ambapo imedai kuwa watuhumiwa hao walimuua kwa makusudi, Bi. Nicodemu kinyume
na kifungu cha 196 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Akisoma hukumu yao, Jaji Munisi ambaye
alianza majira ya saa 14:21 mchana na kukamilisha saa 15:26 ameisema katika
kesi hiyo upande wa mashtaka na utetezi haubishaniwi kuhusu kifo cha marehemu.
Alisema katika kutetea hoja zao upande
wa mashtaka ulileta mashahidi 6 ambao wote kwa pamoja wakiongozwa na shahidi namba
moja waliwatuhumu washtakiwa kuhusika na tukio hilo.
Alinukuu kielelezo namba Moja
kilichowasilishwa na hakimu mkazi wa mahakama ya mwanzo Usseri ambaye
alimwandikia maelezo ya ungamo ambapo Mshtakiwa namba tatu alikiri kuwa yeye na
wenzake wawili walienda nyumbani kwa marehemu majira ya saa tatu usiku kwa
ajili ya kwenda kumdai fedha yao kiasi cha tsh 9600 ikiwa ni malipo yao ya
kupukuchua mahindi lakini walipofika walimkosa nyumbani na hivyo wakapanda
ukuta wa nyumba na kuingia ndani ambapo walijificha uvunguni mwa kitanda chake
na aliporudi walimshambulia kwa mapanga na kusabababisha kifo chake.
Kutokana na ushahidi huo alisema
Mshtakiwa namba moja na namba mbili wanatiwa hatiani kuhusika moja kwa moja na
mauaji kutokana na ukiri wao kwa mlinzi wa amani, Mchukua maelezo na shahidi
namba tatu ambaye ni mume wa marehemu ambaye anadai kuwa alishuhudia
wakitekeleza tukio hilo na kuwatambua wahusika Kutokana na utetezi huo, Jaji
Munisi alisema ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kuthibitisha kuhusika pasipo
shaka kwa washtakiwa wote watatu kwa mujibu wa sheria kifungu cha 197 ya sheria
ya kanuni ya adhabu washtakiwa hao adhabu yao ni kunyongwa hadi kufa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WALIOUA KWA DENI LA SHILINGI 9,600 WANYONGWA WILAYANI ROMBO.”
Post a Comment