Saturday, July 26, 2014
WATALII WAVAMIWA HOTELINI NA KUPOKEA KICHAPO KISHA KUPORWA LAPTOP, KAMERA, SIMU NA FEDHA
Do you like this story?
Kundi la watu wanaoaminika kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za moto na mapanga, wamevamia watalii 17 kutoka mataifa mbalimbali na kuwapora kiasi kikubwa cha fedha, kamera na kompyuta mpakato (Laptop), kisha kuwajeruhi wanne na kutoweka.
Tukio hilo
kubwa kuwahi kutokea siku za hivi karibuni mkoani Kilimanjaro, limetokea juzi
alifajiri eneo la Mailisita kwenye hoteli ya kitalii ya Weruweru River Lodge
inayomilikiwa na mfanyabiashara Cuthbert Swai, ambaye pia anamiliki kampuni ya
wakala wa utalii ya Ahsante Tours ya mjini hapa.
Kwa mujibu
wa mashuhuda wa tukio hilo, watalii hao kutoka mataifa mbalimbali, walikumbwa
na mkasa huo wakiwa wamelala ndani ya mahema majira ya saa 9 alfajiri, ambako
walitishwa kwa bunduki na mapanga kabla ya kuporwa mali zao.
Katika
tukio hilo, watalii watatu waliporwa zaidi ya dola 2,090 za Marekani, mmoja
pauni 110 za Uingereza na euro kiasi kisichojulikana, sh milioni 5.4, kamera
zaidi ya nne na moja ikiwa na thamani ya sh milioni 1.5 na nyingine ikiwa na
thamani ya dola 3,000 za Marekani, zaidi ya sh milioni 4.5.
Habari
kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zilizothibitishwa na Kamanda wa Mkoa Kilimanjaro,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Robert Boaz, majambazi hao kabla ya
kufanya uhalifu huo, waliwakusanya watalii hao eneo moja na kuanza kuwapora
kila kitu walichokuwa nacho.
Hata
hivyo, Kamanda Boaz hakuweza kulizungumzia tukio hilo kwa kina, ikiwamo kutaja
majina ya watalii hao, uraia wao na thamani halisi ya mali walizoporwa,
kutokana na kuwa katika pilikapilika za kwenda uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Kilimanjaro (KIA), kupokea ugeni wa Spika wa Bunge la Nigeria.
Kamanda
Boaz, aliwaambia waandishi wa habari waliofika ofisini kwake jana kuwa tukio
hilo atalitolea maelezo kamili leo kutokana na kutingwa na ugeni huo.
Ofisa
mmoja wa polisi aliyeomba kutotajwa jina lake, alisema kuwa miongoni mwa
watalii hao walioporwa mali zao, wako wanne waliokuwa wakijiandaa kuondoka na
ndege alfajiri hiyo kupitia KIA.
Aliongeza
kuwa watalii hao walijikuta katika mkasa huo, baada ya dereva wa gari
lililokuwa limewabeba kuwashwa kuashiria kuondoka hotelini hapo, ndipo
majambazi hao walipolivamia na kuanza kuwashambulia na hatimaye kuwapora mali
zao ingawa watalii hao waliendelea na safari yao.
Mmoja wa
wakurugenzi wa hoteli hiyo, Stella Shangali alipoulizwa juu ya tukio hilo,
hakukiri wala kukanusha kuwapo, zaidi ya kumtaka mwandishi kuwasiliana na
kamanda wa mkoa kwa ufafanuzi zaidi.
Credit: Tanzania Daima
Credit: Tanzania Daima
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WATALII WAVAMIWA HOTELINI NA KUPOKEA KICHAPO KISHA KUPORWA LAPTOP, KAMERA, SIMU NA FEDHA ”
Post a Comment