Thursday, August 14, 2014
EBOLA SIYO MCHEZO_MGONJWA AZUA KIZAA ZAA HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA, WAUGUZI,MADAKTARI WATIMUA MBIO
Do you like this story?
Kufuatia kuzuka kwa ugonjwa hatari wa Ebola katika nchi
jirani ya Rwanda mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt,Ntuli Kapologwe
amewatoa hofu wananchi wa mkoa wa Shinyanga juu ya uvumi wa kuingia kwa ugonjwa
hatari wa Ebola mkoani Shinyanga.
Mganga huyo wa mkoa amewatoa hofu wananchi kufuatia kuenea
uvumi kuwa kuna mgonjwa wa Ebola aliyefikishwa katika hospitali ya mkoa wa
Shinyanga kutoka moja ya mitaa katika Manispaa ya Shinyanga.
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu huyo mgonjwa huyo ambaye alikuwa
akitokwa damu mdomoni na puani alifika hospitalini hapo Agosti 12 mwaka huu na
mara baada ya kufika wauguzi na madakitari walitaharuki.
Mgonjwa alilazimika kupelekwa chumba cha wagonjwa mahututi
(ICU) huku baadhi ya wauguzi na madaktari wakimkimbia hali iliyotia hofu kwa
baadhi ya wahudumu na hata wagonjwa hospitalini hapo.
Hata hivyo Mganga Mkuu huyo alisema hakuna mgonjwa wa Ebola
na kuwataka wananchi waamini hivyo na kuwa uongozi wa mkoa umejipanga
kukabiliana na ugonjwa.
Alisema mgonjwa aliyepokelewa ana matatizo ya kutokwa damu
mara kwa mara na kuwa baada ya uchunguzi wa awali imebainika siyo Ebola.
Hata hivyo katika kukabaliana na ugonjwa huyo waganga
wakuu katika halmashauri zote 6 za wilaya za mkoa wamekubaliana pindi
atakapogundulika mtu mwenye dalili za ugonjwa huo taarifa itolewe mara moja
katika ngazi ya mkoa na kuna timu maalum ya kushughulika na ugonjwa huo hatari.
Alisema mara baada ya taarifa kutolewa timu hiyo ndiyo
itakayo thibitisha kama kweli mgojwa huyo ana dalili zote za ebola na taarifa
kutolewa.
Mganga huyo pia alisema hospitali zote katika halmashauri za
mkoa wa Shinyanga zimepewa maelekezo juu ya kukabiliana na ugonjwa huo.
Na Kadama Malunde-Shinyanga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ EBOLA SIYO MCHEZO_MGONJWA AZUA KIZAA ZAA HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA, WAUGUZI,MADAKTARI WATIMUA MBIO”
Post a Comment