Thursday, August 14, 2014
MWENYEKITI WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA ASEMA KATIBA ITAKUWA NI YA MAKUNDI YOTE.
Do you like this story?
Na
Magreth Kinabo
Mwenyekiti
wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta amewahakikishia Watanzania
kwamba Katiba Mpya itakayopatikana itakuwa imezingatia matakwa ya makundi
mbalimbali.
Mhe .
Sitta aliyataja makundi hayo baadhi ya makundi hayo kuwa ni
wafugaji, wakulima, wavuvi na wasanii.Huku akisema Katiba Mpya itakayopatikana
itakuwa ni bora kuliko iliyopo sasa.
Kauli hiyo
ilitolewa jana na Mhe . Sitta wakati akizungumza na wafugaji wapato 44 kutoka
mikoa mbalimbali,ambao waliongozwa na Mwenyekiti wa ujumbe huo, Huruma Ole
Kalaita na Mlezi wao, ambaye mjumbe wa Bunge hilo na Mbunge wa Jimbo la Maswa
Magharibi(CHADEMA).
“Tunaamini
ni wakati wa Katiba Mpya… lazima iweze kupatikana. Itakayozingatia Sheria bora
na maslahi ya makundi mbalimbali yatapatikana.
“ Utungaji
wa Katiba ni suala la wananchi kutanguliza suala la muundo wa Serikali si haki.
Ni muhimu kutanguliza haki za raia. Kinachotangulia ni haki za raia wetu na
makundi mbalimbali,” alisisitiza Mhe. Sitta.
Aidha Mhe.
Sitta aliwakikishia wafugaji hao,kwamba Bunge hilo “ liko hapa kisheria kwa
kanuni zake linaendelea na wale wanaopiga kelele hawalitakii mema taifa letu
kwa sababu demokrasia yoyote ni kupata kura ya walio wengiu,” alisema.
Kwa
upande wake Mlezi wa wafugaji hao, Mhe. Shibuda alimpongeza Mhe. Sitta kwa
jitihada zake za kuendeleza vikao vya Bunge hilo, ambapo pia alimsihii
kuwa asikatishwe tamaa kwa dhamira yake njema ya kuendelea kuongoza vikao
vya Bunge hilo.
Akizungumzia
kuhusu masuala ya wafugaji hao na wakulima wa zao la pamba nchini, alisema kuwa
wako pamoja naye.
“ Hivi
Serikali tatu au mbili inatiririsha nini kwa wakulima na wafugaji. Tunataka
viongozi wa kukabiliana na matatizo ya wananchi,” alisisitiza Shibuda.
Kwa
upande Mwenyekiti wa wafugaji hao, Kalaita alipendekeza Katiba Mpya,
itamke matumizi bora ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji ili kuondoa migogoro
ya wakulima na wafugaji.
Makamu
wa Mwenyekiti wa wafugaji hao, Kasundwa Wamalwa kutoka Kanda ya Magharibi
akisoma mapaendekezo ya risala yao waliyoiwasilisha kwa Mwenyekiti wa Bunge
hilo, Mhe. Sitta, ambapo walipendekeza Katiba Mpya itambue wafugaji wa asili.
Aidha
Makamu Mwenyekiti huyo aliwataka wajumbe wa Bunge hilo, kuwa na hofu ya
Mwenyezi Mungu wakati wanapoendelea na mchakato huo.
Miongoni
mwa makundi mengine waliofika katika ofisi za Bunge mjini Dodoma ni Jukwaa la
Katiba (JUWAKATA) na Jukwaa la Wahariri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWENYEKITI WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA ASEMA KATIBA ITAKUWA NI YA MAKUNDI YOTE. ”
Post a Comment