Thursday, August 7, 2014
MPIGA DEBE MAARUFU IRINGA ACHOMWA KISU KISA SHILINGI ELFU 2.
Do you like this story?
DENI
la Sh 2,000 limetosha kumaliza uhai wa mpiga debe maarufu wa stendi ya mabasi
yaendeayo mikoani ya mjini Iringa, Samwel Yengayenga baada ya kuchomwa kisu
mara mbili katika eneo la mgongoni na kifuani.
Tukio
hilo la kinyama limetokea jana majira ya saa 6:.55 mchana baada ya Yengayenga
na mtuhumiwa wa mauaji yake aliyekuwa akidai kiasi hicho cha fedha kurushiana
maneno makali na kisha kupigana.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi
alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Festo Ruben Mkalala (26), muosha magari, mkazi
wa mjini Iringa ambaye alikamatwa mara baada ya kufanya tukio hilo.
Mungi
alisema Yengayenga, Mkalala na mtu mwingine wa tatu (hakumtaja jina) wanadaiwa
siku nne zilizopita waliosha basi la Kimotco linalofanya safari zake kati ya
Iringa na Arusha.
“Stahiki
ya kazi hiyo ilikuwa Sh 15,000; hata hivyo hawakulipwa fedha hizo baada ya
kumaliza kazi hiyo,” alisema.
Alisema
siku iliyofuata Mkalala na kijana huyo mwingine waliyefanya naye kazi
walikwenda kuchukua ujira wao na kugawana Sh 5,000 kila mmoja huku Mkalala
akiahidi kutunza Sh 5,000 za Yengayenga mpaka watakapokutana.
Walipokuta,
RPC alisema Mkalala alimpa Yengayenga Sh 3,000 badala ya Sh 5,000 na kuahidi
kummalizia kiasi kilichobaki kesho yake.
Kitendo
hicho kwa mujibu wa mashuhuda kinadaiwa kumchukiza Yengayenga aliyeamua
kunyanganya simu ya Mkalala mpaka amaliziwe Sh2,000 zake zilizobaki.
Kamanda
Mungi alisema Mkalala alichukizwa na uamuzi huo na kuanzisha ugomvi uliopeleka
kifo cha Yengayenga.
“Uchunguzi
wa awali unaonesha Mkalala aliamua kupigana na Yengayenga ili arudishiwe simu
yake na alipozidiwa alikimbia kusikojulikana na kurudi akiwa na kisu mkononi,”
alisema.
Ili
kuipata simu yake, Kamanda Mungi alisema ushahidi wa awali unaonesha Mkalala
alitumia kisu hicho kumchoma mgongoni na kifuani Yengayenga na kusababisha
mauti yake.
Yengayenga
alikufa papo hapo katika tukio ambalo mtuhumiwa huyo alikamatwa na kufikishwa
kituo cha Polisi cha kati cha mjini Iringa.
Na Frank
Leonard -Iringa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MPIGA DEBE MAARUFU IRINGA ACHOMWA KISU KISA SHILINGI ELFU 2.”
Post a Comment