Rais Jakaya Mrisho Kikwete na
Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika na
wake zao, Mama Salma Kikwete na Mama Getrude Mutharika, wakiongea kwa furaha walipokutana kwenye
hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC,
Marekani. Rais Kikwete na Rais Mutharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika
walioalikwa kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa
Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa
Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo
mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.
PICHA NA IKULU
|
0 Responses to “RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS WA MALAWI PROFESA PETER MUTHARIKA JIJINI WASHINGTON DC, MAREKANI.”
Post a Comment