Thursday, August 7, 2014
RUFANI YA 'NG'ATANG'ATA' LUIS SUAREZ KUSIKILIZWA KESHO CAS.
Do you like this story?
MWANASHERIA wa Luis Suarez anajiamini
kuwa adhabu ya kifungo cha miezi minne cha mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez
itapunguzwa na mahakama ya juu ya rufani ya michezo ya CAS ambapo rufani hiyo
itasikilizwa kesho ijumaa.
Suarezi alikata rufaa kupinga adhabu ya
kufungiwa shughuli zote za soka na FIFA na rufani yake itasikilizwa Agosti 8
mwaka huu katika mahakama hiyo iliyopo Lausananne, Uswizi.
Nyota huyo mwenye miaka 27 alifungiwa
baada ya kumng’ata beki wa Italia,Giorgio Chiellini wakati akiichezea Uruguay
katika mechi ya kombe la dunia nchini Brazil na baada ya tukio hilo alijiunga
na Barcelona kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 75 kutokea Liverpool.
Rufani aliyowasilishwa FIFA na Suarez
alitupiliwa mbali mwezi uliopita na akaamua kukata rufani mahakama ya juu ya
rufani ya michezo.
Maamuzi ya CAS yanatarajia kutolewa
wiki ijayo. Kama atashinda maana yake Suarez ataanza mazoezi na wachezaji
wenzake wiki mbili zijazo na atakuwepo katika mechi ya ya kwanza ya msimu mpya
wa La Liga dhidi ya Elche, jumapili ya Agosti 24 mwaka huu.
Shirikisho la soka la Uruguay (UAF)
lilimteua wakili wa Brazil, Daniel Cravo ili asimamie rufani dhidi ya kifungo
ambacho kimemfanya Suarez akose mechi 9 za kimataifa. Mchezo mmoja wa kifungo
umepita ambao ulikuwa dhidi ya Colombia hatua ya 16 ya kombe la dunia.
Cravo aliiambia Radio Globo
akiwa Brazil kuwa anaamini adhabu hiyo itapunguzwa.
“Nadhani FIFA walitaka kuonesha kuwa
wanaweza kuchukua hatua,” alisema.” Maamuzi hayakuridhisha ukilinganisha na
matukio makubwa yaliyowahi kutokea huko nyuma. Hata kifungo cha (Zinedine)
Zidane mwaka 2006 au yale ya Leonardo na (Mauro) Tassotti mwaka 199, adhabu
haikuwa kubwa zaidi”.
“Tukio la Suarez ndio baya zaidi kuwahi
kutokea katika historia ya kombe la duniua?
“Naamni kifungo kitakachoathiri kazi
yake kwa ngazi ya klabu kitaondolewa. Hakuna kesi iliyoamuriwa kama hiyo katika
historia.
“Naenda kujaribu na kupunguza kifungo
cha kuichezea Uruguay—mechi tisa ni nyingi sana na zinaweza kumzuia kucheza
mpaka 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RUFANI YA 'NG'ATANG'ATA' LUIS SUAREZ KUSIKILIZWA KESHO CAS.”
Post a Comment