Friday, August 1, 2014
UGANDA YAFUTA SHERIA DHIDI YA USHOGA.
Do you like this story?
Wanaume wanaounga mkono mapenzi ya jinsia moja Uganda |
Baadhi ya waandamanaji waliounga mkono serikali kwa kuharamisha mapenzi ya jinsia moja. |
Mahakama ya kikatiba nchini Uganda imefutilia mbali sheria dhidi ya
wapenzi wa jinsia moja ambayo ilisababisha mataifa ya magharibi kuinyima
msaada.
Kadhalika
sheria hiyo ilizua gumzo sana sio tu Uganda bali kote duniani ambapo mataifa ya
Magharibi yalilazimika kuingilia kati.
Mahakama
ilisema kuwa mswada huo kabla ya kuidhinishwa kuwa sheria ulipitishwa na
wabunge ambao idadi yao haikutosha kupitisha mswada na kwa hivyo ni kinyume na
sheria.
Vitendo
vya mapenzi ya jinsia moja, tayari vilikuwa vimeharamishwa Uganda , lakini
sheria hiyo mpya pia iliharamisha hatua zozote za kueneza mapenzi ya jinsia
moja na wakati huu hata kuwajumuisha wanawake wasagaji kama sehemu ya wapenzi
wa jinsia moja.
Mataifa
kadhaa ya Magharibi yamesitisha msaada kwa Uganda hasa baada ya sheria hiyo
mpya kupitishwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UGANDA YAFUTA SHERIA DHIDI YA USHOGA.”
Post a Comment