Friday, August 1, 2014
WAZIRI WA MAZINGIRA DKT BINILITH MAHENGE AZINDUA TOVUTI YA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI.
Do you like this story?
sehemu ya wadau waliyoudhulia katika mkutano huo kushuhudia makubaliano ya mkataba huo. |
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula wakipeana Mkataba na mkuu msaidizi wa wa chuo cha kilimo SUA Prof. Gerald Monella baada ya kusaini. |
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Mh. Dkt. Eng Binilith Satano Mahenge
akizindua rasmi tovuti ya mabadiliko ya tabianchi itakayotumika kutoa taarifa
mbalimbali za utunzaji wa Mazingira.
Mheshimiwa
Eng Dkt. Binirithi S. Mahenge
(mbunge) Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais (mazingira) azindua
tovuti ya mabadiliko ya tabia nchi. Katika hotuba yake fupi ya uzinduzi
wa tovuti hiyo, aliyoandaliwa kwa ufadhili wa serikali ya Denmark Mh.
Binirithi Mhenge amesema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi huangaliwa kwa
muda wa miaka 30 hivyo kwa kipindi hiki chote kumekuwa na madhara mengi
yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabia Nchi ikiwa ongezeko la joto, kina
cha bahari kuongezeka pamoja na ongezeko la majanga ya mvua zisizo na
viwango, kutoka na shughuli za binadamu katika uzalishaji hasa viwanda
vikubwa
Alisema kwa
tovuti inayozinduliwa ina umuhimu mkubwa kwani inaelezea maeneo ya hali ya
mabadiliko ya tabia nchi na juhudi za serikali katika kukabiliana na
athari zinazoletwa na mabadiliko hayo.
“ziko sababu
za kuungana na wenzetu ili kuondoa tatizo hili la
mabadiliko ya nchi ambapo tovuti hii WWW.climatechange.go.tzinatuunganisha
na tovuti mbali mbali katika kupunguza gesi joto hapanchini pia inaelezea fursa
zilizopo katika miradi na program mbali mbali. Alisisitiza”
Alibaini kuwa
tovuti hii itachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza uelewa na weledi kuhusu
mabadiliko ya tabia nchi nchini kwa wananchi na wadau kwa ujumla.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WAZIRI WA MAZINGIRA DKT BINILITH MAHENGE AZINDUA TOVUTI YA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI.”
Post a Comment