Thursday, September 4, 2014
DAVID MWAMWAJA: LENGO LETU MSIMU UJAO NI KUIRUDISHA JUU PRISONS.
Do you like this story?
Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
David Mwamaja
hajafanya usajili mkubwa licha ya kikosi chake kupambana hadi dakika ya mwisho
msimu uliopita ili kusalia katika ligi kuu.
Baada ya ushindi wa
bao 1-0 dhidi ya Ashanti United, 24 April, Tanzania Prisons ilifanikiwa kubaki
katika ligi kuu Bara. Wengi walitaraji timu hiyo ingefanya usajili mkubwa
wakati wa dirisha la usajili kwa kuamini kuwa timu hiyo inahitaji mabadiliko
makubwa.
Haijawa hivyo
na Mwamaja ameweza kuhakikisha mchezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar, Amir
Omary anatua katika kikosi chake kwa lengo la kuongeza makali katika safu ya
mashambulizi ambayo ilibebwa zaidi na mshambulizi, Peter Michael na Richard
Peter msimu uliopita.
“ Ligi itakuwa ngumu
msimu ujao, lakini tunataka kuirudisha juu Tanzania Prisons kama ilivyokuwa
enzi za kina Osward Morris.Nimeongezwa katika timu hii kwa lengo la kusaidiana
na wachezaji waliopo ili kuifanya Prisons kuwa timu bora msimu ujao.. Tangu
nimefika hapa nimepata vitu vingi vipya ndani na nje ya uwanja. Upendo,
ushirikiano na umoja ni mambo yaliyotawala hapa” anasema mshambulizi, Amir
Omary ambaye amesajiliwa akitokea klabu iliyoshuka daraja ya JKT Oljoro.
Michael alifunga
mabao 12 msimu uliopita, Richard alifunga mabao manne na Amir alifunga mabao sita
katika kikosi cha Oljoro msimu uliopita na mchexzaji huyo wa Zanzibar Heroes
anaamini kuwa umoja wao utawasumbua walinzi wengi msimu wa 2014/15.
“ Ni safu kali ya
mashambulizi, kila timu imejiandaa msimu ujao lakini nachoweza kusema
tumejipanga kuhakikisha Prisons inafanya vizuri msimu ujao. Mwalimu yoko poa na
kila mmoja kikosini anafahamu ni kitu gani ambacho kinatakiwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DAVID MWAMWAJA: LENGO LETU MSIMU UJAO NI KUIRUDISHA JUU PRISONS.”
Post a Comment