Thursday, September 4, 2014
MBEYA CITY KUJIPIMA UBAVU NA BIG BULLETS YA MALAWI
Do you like this story?
Ili kujiimarisha
zaidi kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara, klabu ya Mbeya City
inataraji kucheza michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki kabla ya kuanza kwa
msimu mpya Septemba 20 ambapo timu hiyo iliyomaliza katika nafasi ya tatu msimu
uliopita itafungua dimba dhidi ya ' Maafande' wa JKT Ruvu katika uwanja
wa Sokoine, Mbeya.
Kocha mkuu wa timu
hiyo, Juma Mwambusi ameuagiza uongozi wa timu hiyo kumtafutia michezo miwili
dhidi ya klabu za Malawi.
Big Bullets ni klabu
kongwe nchini Malawi na Kusini mwa bara la Afrika itacheza na City katika
mchezo wa kwanza wa kimataifa.
"
Nimeuambia uongozi wangu nahitaji mechi mbili ngumu za kimataifa na timu kutoka
nchini Malawi. Tunataraji kucheza na Big Bullets ya Malawi ili kujiimarisha
zaidi kabla ya kuanza kwa msimu mpya" alisema, Mwambusi.
City imefanikiwa
kuwabakisha kikosini wachezaji wake nyota kama, Paul Nongwa, Saad Kipanga,
Hassan Mwasapili, na golikipa, David Baruani licha ya wachezaji hao kuwaniwa na
timu kubwa katika dirisha la usajili.
Mwagane Yeya, Eric
Banda wataungana na nyota mpya, Themi Felix kuifanya timu hiyo kuendelea kuwa
bora katika msimu wake wa pili katika ligi ya Tanzania Bara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MBEYA CITY KUJIPIMA UBAVU NA BIG BULLETS YA MALAWI”
Post a Comment