Thursday, September 4, 2014
SERIKALI YASITISHA VIBALI VYA MATANGAZO YA NTIBA ZA ASILI.
Do you like this story?
Dar es Salaam.
Serikali imesitisha vibali vya kurusha matangazo ya tiba za asili na mbadala
kwenye vyombo vyote vya habari baada ya kubaini kuwa yanapotosha jamii.
Taarifa iliyotolewa
na Baraza la Tiba za Asili na Tiba Mbadala kwa vyombo vya habari jana, inaeleza
kuwa katika siku za karibuni kumekuwapo na matangazo mbalimbali ya tiba hizo
ambayo baadhi yake hayaisaidii jamii.
Kutokana na taarifa
hiyo ya baraza, vyombo vya habari havipaswi kupokea kibali chochote cha
kutangaza matangazo ya tiba hizo hivi sasa, kwa kuwa ni batili.
“Hivyo basi kituo
chochote cha redio, luninga, mitandao na magazeti hayaruhusiwi kurusha tangazo
lolote linalohusiana na mambo ya tiba asili na mbadala kwa kipindi hiki,”
ilisema taarifa iliyosainiwa na Lucy Mziray.
Pia taarifa hiyo
inaeleza kuwa, chombo chochote kitakachorusha tangazo au kipindi kitatozwa
faini na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Akizungumzia uamuzi
wa Serikali uliochukuliwa, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk
Primus Saidia alisema kuwa matangazo ya tiba mbadala na asili kwa muda mrefu
yamekuwa yakipotosha umma kwa kukiuka Sheria ya Waganga na Tiba Mbadala ya
mwaka 2002 inayowazuia kujiita madaktari na kujitangaza kwenye vyombo vya
habari.
“Wanakwenda kinyume
wanajiita madaktari, wengine maprofesa, halafu wanakwenda mbali zaidi na kuvaa
vifaa vya udaktari kwenye televisheni ili kuwavutia watu,” alisema Dk Saidia.
Aliongeza: “Kuna watu
wanatangaza kuwa wanatibu figo kwa siku saba jambo ambalo haliwezekani duniani
kote, wanachofanya ni kuwachelewesha wagonjwa kwenda hospitali mapema.”
Naye mtaalamu wa tiba
za asili, John Kidua, alisema serikali imefanya kosa kuyazuia matangazo yote
badala ya kuwaadhibu watu waliobainika kuipotosha jamii pekee yao.
Alisema upo
uthibitisho kuwa baadhi ya dawa za asili zinatibu vizuri kuliko dawa za
hospitali jambo ambalo limekuwa kikiokoa fedha nyingi za kuwasafirisha wagonjwa
nje ya nchi.
“Ilitakiwa serikali
itoe msaada kwetu ili tuongeze nguvu pale tunaposhindwa na siyo kutujumuisha
wote kwenye kikapu kimoja,” alisema Kidua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SERIKALI YASITISHA VIBALI VYA MATANGAZO YA NTIBA ZA ASILI.”
Post a Comment