Thursday, September 4, 2014
HATIMA YA BUNGE LA KATIBA MIKONONI MWA JK.
Do you like this story?
Dodoma. Hatima
ya Bunge Maalumu la Katiba imebaki mikononi mwa Rais Jakaya Kikwete, ambalo
limemwandikia barua kiongozi huyo wa nchi kutaka ufafanuzi wa kisheria kuhusu
tarehe ya mwisho ya kumaliza vikao vyake.
Hiyo ni
kutokana na muda uliopangwa kwenye ratiba ya bunge hilo kuzua utata wa kisheria
na kuwapo uwezekano wa mwingiliano na Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la
Wawakilishi (BLW), Zanzibar.
Ratiba ya
Bunge Maalumu la Katiba inaonyesha kuwa limepanga kuhitimisha vikao vyake
mwishoni mwa Oktoba, tofauti na tarehe iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete Julai
28, mwaka huu ambayo ilitangazwa katika Gazeti la Serikali (GN) namba 254 la
Agosti Mosi.
Tangazo la
Rais linaonyesha kuwa awamu ya pili ya Bunge Maalumu ingeanza Agosti 5, 2014 na
kumalizika Oktoba 4, lakini ratiba ya Bunge hilo inaonyesha kuwa litamalizika
Oktoba 31, siku ambayo mwenyekiti wa Bunge hilo atakabidhi kwa Rais Katiba
inayopendekezwa.
Hata hivyo,
uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa hadi sasa Serikali bado haijatoa tangazo
(GN) lingine kuongeza muda hadi mwishoni mwa Oktoba kama alivyosema Mwenyekiti
wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta wakati akitoa ufafanuzi wa siku 60 zilizotengwa
kwa ajili ya Bunge hilo, Agosti 5 mwaka huu.
Sitta alisema
kwa kadiri ya tafsiri, siku za kazi ni Jumatatu hadi Ijumaa ambazo wajumbe
wanapaswa kufanya kazi na kwamba Jumamosi na Jumapili siyo sehemu ya siku 60
zilizoongezwa na Rais.
Hata hivyo,
Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad alisema hadi sasa hawajapata
maelekezo ya ziada kutoka serikalini ambako waliandika barua ya kuomba
ufafanuzi wa kisheria kuhusu suala hilo.
“Tulimwandikia
barua, Katibu Mkuu Kiongozi (Ombeni Sefue) kuomba ufafanuzi wa siku hizo kama
ambavyo sisi tungependa iwe, lakini hadi sasa bado hatujajibiwa lakini bado
siku zipo nadhani tutajibiwa tu wakati mwafaka,” alisema Hamad ambaye pia ni
Katibu wa Baraza la Wawakilishi.
Sefue alikiri
ofisi yake kupokea barua kutoka Bunge Maalumu ikiomba ufafanuzi ambao
ungeliwezesha kuongeza siku kwa lengo la kukamilisha kazi ya kujadili na
kuandika Katiba inayopendekezwa na kwamba maombi yao bado yanafanyiwa kazi.
“Bado tuna
muda wa kutosha tu, ni kweli tulishayapokea maombi ya Bunge Maalumu kuhusu
suala hilo na Mheshimiwa Rais akikamilisha kazi yake watajulishwa tu,”alisema
Sefue.
Licha ya ahadi
iliyotolewa na Sitta ni dhahiri kwamba suala hilo lina utata wa kisheria
kutokana na kauli iliyowahi kutolewa na Mwanasheria wa Serikali (AG), Jaji
Frederick Werema wakati akitoa ufafanuzi wa maana ya siku 70 ambazo Bunge
lilikaa mara ya kwanza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HATIMA YA BUNGE LA KATIBA MIKONONI MWA JK.”
Post a Comment