Saturday, July 19, 2014

NAIBU WAZIRI WA UJENZI ENG.GERSON LWENGE AKAGUA BARABARA ZA KUELEKEA KWENYE MACHIMBO YA CHUMA NA MAKAA YA MAWE WILAYA YA LUDEWA MKOANI NJOMBE






Na Gabriel Kilamlya Ludewa

Serikali Imesema Itawachukulia Hatua za Kisheria Wakandarasi Wanaotekeleza Miradi wa Upanuzi wa Barabara ya Ludewa Kuelekea Migodi ya Chuma ya Liganga na Makaa ya Mawe ya  Mchuchuma  Watakaoshindwa Kutekeleza Kwa Wakati na Chini ya Kiwango .

Akizungumza Katika  Ziara ya Siku Mbili ya Kikazi ya Kukagua  Maendeleo ya Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara Wilayani Ludewa, Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge Amesema Amebaini Kuwepo Kwa Kasi Ndogo Kwa Baadhi ya Wakandarasi Wanatengeneza Barabara Hizo Licha ya Serikali Kuwalipa Fedha za Kutosha Kwa Ajili ya Shughuli Hiyo.

Amesema Serikali Inatambua Umuhimu wa Barabara Hizo na Kwamba Kukamilika Kwake Kutasaidia Kukuza Uchumi wa Taifa na Wananchi wa Wilaya ya Ludewa na Mkoa wa Njombe Kutokana na Madini Yatakayochimbwa Katika Migodi ya Liganga na Mchuchuma.

Akizungumza Kwaniaba ya Meneja wa TANROADS Mkoa wa Njombe Mhandisi Daniel Kindole Amesema Mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Ludewa Kuelekea Migodi ya Chuma ya Liganga na Makaa ya Mawe ya Mchuchuma Inaendelea Vizuri na Kuongeza Kuwa Huenda Ikashindwa Kukamilika Kwa Wakati Inatakiwa Kukamilika Julai 30 Mwaka Huu Kwa Mujibu wa Mkataba.

Ziara ya Naibu Waziri Mhandisi Lwenge Amefika Hadi Kwenye Makaa ya Mawe Pamoja na Eneo Lenye Chuma Huko Liganga na Kushuhudia Utajiri Mkubwa Uliopo Katika Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Licha ya Wakazi Wake Kuonekana Wakiishi Katika Maisha Duni.

0 Responses to “NAIBU WAZIRI WA UJENZI ENG.GERSON LWENGE AKAGUA BARABARA ZA KUELEKEA KWENYE MACHIMBO YA CHUMA NA MAKAA YA MAWE WILAYA YA LUDEWA MKOANI NJOMBE ”

Post a Comment

More to Read