Wednesday, September 24, 2014
KATIBA MPYA:BUNGE KUTUMA OFISA SAUDIA KUSIMAMIA KURA
Do you like this story?
Dodoma. Ofisi ya Bunge la Katiba itamtuma ofisa wake
kwenda Makka, Saudi Arabia kusimamia upigaji kura kupitisha Katiba
inayopendekezwa kwa wajumbe wa Bunge hilo wanaokwenda Hijja.
Hayo
yalielezwa jana na Katibu wa Bunge hilo, Yahya Khamis Hamad alipotakiwa kueleza
idadi kamili ya wajumbe wa Bunge hilo wanaotarajiwa kuwa nje ya nchi na jinsi
watakavyopiga kura.
Juzi, Bunge
hilo lilizifanyia marekebisho kanuni zake ili kuwaruhusu wajumbe watakaokuwa
nje ya Ukumbi wa Bunge wakiwamo wanaokwenda Hijja kuipigia kura Katiba
inayopendekezwa, iliyokabidhiwa kwa Kamati ya Uongozi jana.
Chini ya
marekebisho hayo, mjumbe aliye nje ya Bunge, ataruhusiwa kupiga kura ya wazi au
ya siri kwa njia ya fax au mtandao kama itakavyoelekezwa na katibu kwa
kushauriana na mwenyekiti.
Hamad alisema
hadi kufikia jana mchana walikuwa wamewatambua wajumbe wanane ambao watakwenda
Hijja huko Uarabuni lakini orodha ya watakaokuwa nchi nyingine bado
haijajulikana.
Hamadi alisema
ofisa wake huyo atasimamia kura za wajumbe wanaokwenda Hijja katika upigaji
kura unaotarajiwa kuanza Septemba 29 hadi Oktoba 2 mwaka huu.
Alisema ni
vigumu kutaja vituo watakavyopigia kura sasa kwa sababu bado hawajawauliza
wajumbe wengine waliopo nje ya nchi ambao wangependa kupiga kura wakiwa huko.
Kuhusu iwapo
watapiga moja kwa moja kwa mtandao au watapiga kwenye karatasi na kutoa vivuli,
Hamad alisema suala hilo litaamuliwa na Kamati ya Uongozi ya Bunge chini ya
Mwenyekiti, Samuel Sitta.
Ukawa
wapinga
Wenyeviti
wenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Profesa Ibrahim Lipumba na James
Mbatia wamelishukia Bunge hilo kwa kuruhusu upigaji kura nje ya nchi.
Akizungumza
jana, Profesa Lipumba alisema kilichofanywa na Sitta na wajumbe wake ni
uchakachuaji unaoweza kuliingiza Taifa kwenye mgogoro mkubwa.
“Kwanza
taratibu za kura mabunge ya Jumuiya ya Madola ni kura zote zinapigwa ndani ya
Bunge. Unapozungumzia akidi imetimia ni wajumbe walioko ndani ya Bunge,”
alisema Profesa Lipumba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “KATIBA MPYA:BUNGE KUTUMA OFISA SAUDIA KUSIMAMIA KURA”
Post a Comment