Tuesday, September 23, 2014
MAAJABU: AMKODISHA MPENZI WAKE KWA MTU YEYOTE ILI APATE PESA YA KUNUNUA IPHONE 6
Do you like this story?
Mwanafunzi wa Chuo kikuu kimoja cha
China ambaye jina lake halikutambulika kwa haraka ameamua kufanya ‘uchizi’ ili
mradi tu aipate pesa ya kununua aina mpya ya iPhone iliyoingia sokoni, iPhone6.
Kijana huyo wa alionekana akiwa nje ya
chuo kikuu cha Songijiang akiwa na bango kubwa lililoandikwa kwa kichina na
kutafsiriwa ‘Girlfriend Sharing’.
Katika tangazo hilo kijana huyo
anaeleza kuwa yuko tayari kumkodisha mpenzi wake kwa mtu yeyote atakayeweza
kutoa pesa ili jamaa apate kiasi cha kutosha kuinunua iPhone 6 yenye screen
kubwa.
Picha ya kijana huyo imesambaa kwa kasi
katika mtandao wa kijamii unaotumiwa na wachina uitwao ‘Weibo’ ambao ni kama
Twitter.
Tangazo hilo limeambatana na picha za
mpenzi wake na amewatoa hofu wateja wanaosita kuingia nae mkataba kuwa hata
mpenzi wake ameridhia na yuko tayari kudate na mtu yeyote atakaejitokeza.
Muda wa kuwa na msichana huyo baada ya
kumkodi umebainishwa kutokana na malipo yatakayofanywa na mteja. Viwango ni vya
saa 1 (10 yuan), siku 1 (50 yuan) au mwezi mmoja (500 yuan).
Hata hivyo, wapenzi hawa sio wa kwanza
kujiweka sokoni ili wapate bidhaa ya kampuni ya Apple. Mwaka jana katika
uzinduzi wa iPhone 5, wanandoa wa Shaghai waliwaweka sokoni watoto wao watatu
ili wapate pesa ya kununua computer na simu za iphones lakini walikamatwa na
kufunguliwa mashitaka.
Lakini pia kijana mdogo wa Hunan alijitolea
kuuza figo lake ili apate pesa ya kununua iPad na iPhone.
Siyo hayo tu, hivi karibuni mwanaume
mmoja wa Saudi Arabia ametaka kupewa iPhone 6 kama mahari ya dada yake hata
kabla aina hiyo ya simu haijazinduliwa Bahrain.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “MAAJABU: AMKODISHA MPENZI WAKE KWA MTU YEYOTE ILI APATE PESA YA KUNUNUA IPHONE 6 ”
Post a Comment