Tuesday, September 23, 2014
MCHEZAJI AFARIKI DUNIA UGANDA KUFUATIA BAO LA FRENK LAMPARD
Do you like this story?
Fahad Musana, ambaye ni shabiki wa
kutupwa wa klabu ya soka ya Chelsea, amefariki dunia baada ya mchezaji wa
zamani wa klabu hiyo, Frank lampard, kuifungia Manchester City bao la
kusawazisha, katika pambano lililopigwa jana baina ya timu hizo mbili.
Musana, mwenye umri wa miaka 24, na
ambaye alikuwa mcheza kandanda la kulipwa nchini Uganda, alikuwa akitizama
mechi hiyo iliyovuta hisia za mashabiki wengi katika kona mbalimbali za dunia,
na alianguka na kuzimia mara baada ya Lampard kusawazisha bao, ikiwa ni dakika
chache sana tangu aingie kutokea benchi, katika dakika za lala salama.
Alithibitishwa kuwa amefariki baada ya
kuwasili katika hospitali ya kijeshi ya Bombo, na rafiki wa karibu wa marehemu
amenukuliwa na vyombo vya habari akisema “Jamaa, amekuwa ni shabiki wa kweli wa
Chelsea, ambaye angeweza kufanya lolote lile kwa ajili ya klabu hiyo. Tulifanya
naye mazoezi asubuhi ya jumapili, na hata mchana tukala chakula cha mchana
pamoja, hakika inasikitisha”
Tukio hili la kusikitisha,
limethibitishwa na Shirikisho la vyama vya soka nchini Uganda (FUFA), ambalo
limetoa tamko lake kufuatia mkasa huu wa kushtusha.
“FUFA, limekumbwa na mshtuko baada ya
kupokea taarifa za kifo cha ghafla cha mchezaji wa klabu ya Simba ya Uganda,
Misana Fahad, katika hospitali ya Bombo. Mwili wa marehemu bado uko hospitalini
hapo, na taratibu za mazishi zinaandaliwa na taarifa zitatolewa baadae”, sehemu
ya taarifa ya FUFA imesomeka hivyo.
Hii si mara ya kwanza kwa mashabiki wa
soka kufariki kufuatia timu wanazozishabikia kushindwa kuibuka na ushindi
katika mechi zao. Kumbukumbu za hivi karibuni sana kwa ukanda wetu wa Afrika
Mashariki na Kati, ni za shabiki mwingine wa soka aliyefariki dunia msimu
uliopita, baada ya timu aliyokuwa akiishabikia ya Manchester United kupoteza
moja ya mapambano yake, ilipokuwa chini ya kocha David Moyes
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “MCHEZAJI AFARIKI DUNIA UGANDA KUFUATIA BAO LA FRENK LAMPARD”
Post a Comment