Tuesday, September 23, 2014
WACHEZAJI MANCHESTER UNITED WAMPOROMOSHEA 'MITUSI' LOUIS VAN GAAL.
Do you like this story?
![]() |
| Angel di Maria alitolewa na Louis van Gaal, United wakiwa 3-3 dhidi ya Leicester |
![]() |
| Di Maria (mstari wa nyuma, katikati) akiwa amekaa benchi na kutazamana United ikipoteza 5-3 |
WAKIWA katika vyumba
vya kubadilishia nguo, wachezaji nyota wa Manchester United walilaumu vikali
kitendo cha Angel di Maria kutolewa katika kipigo cha mabao 5-3 dhidi ya
Leicester.
Di Maria, ambaye
aliifungia United goli la msimu na kuwafanya waongoze 2-0, alikwenda benchi
baada ya kufunga bao la tatu kufanya matokeo yawe 3-3.
Baada ya mechi, moja
ya chanzo habari kutoka Uwanja wa The King Power kimesema kilisikia wachezaji
wa United wakiwaka kweli wakisema: " ‘Why the f*** did we substitute
Di Maria?’. Hatujaona haja ya kutafsiri kwasababu za kimaadili.
Mshambuliaji huyo wa Argentina
alikuwa mchezaji nyota katika mechi dhidi ya QPR wiki iliyopita. Lakini kocha
aliye katika kiti cha moto, Van Gaal, katika dakika ya 76 alimtoa mchezaji huyo
aliyesajiliwa kwa paundi milioni 60 kutokea klabu ya Real Madrid
Leicester kiukweli walipata nafuu
baada Di Maria kutoka na nafasi yake kuchukuliwa na Juan Mata na walifunga
mabao mawili yaliyowapa ushindi mnono.
Van Gaal alimlaumu waziwazi beki
wake wa Kibrazil, Rafael kwa kusababisha penalti katika dakika ya 62.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)



0 Responses to “WACHEZAJI MANCHESTER UNITED WAMPOROMOSHEA 'MITUSI' LOUIS VAN GAAL.”
Post a Comment