Tuesday, September 23, 2014
MWENGE WA UHURU WATEKETEZA SHAHENA YA BANGI WILAYANI RORYA MKOANI MARA.
Do you like this story?
OCD wa Jeshi la Polisi Utegi wilayani Rorya (JINA
LITAKUJIA HIVI PUNDE), amesema mapambano dhidi ya biashara na kilimo cha
bangi wilayani Tarime, moja ya changamoto zake kubwa ni biashara hiyo haramu
kufadhiliwa na wafanyabiashara wakubwa toka nchini Kenya.
OCD aliyasema hayo hivi karibuni, wakati alipokuwa akisimamia uteketezwaji wa kiasi cha tani moja za bangi, zoezi lililofanyika katika eneo maalum la uwanja wa Kituo cha Polisi Utegi. “Bangi inayolimwa Tarime na Rorya inasemekana hufadhiliwa na raia kutoka nchi ya Kenya, lakini tutaendelea kupambana ili kutokomeza biashara ya zao hilo,” alisema .

Pamoja na hayo, aliwashutumu baadhi
ya maofisa wa Jeshi la Polisi wasio zingatia maadili pamoja na baadhi ya
watumishi wa Serikali, kwamba wanajihusisha na biashara hiyo haramu.
“Kuna maofisa wa polisi wasio waaminifu wanavujisha siri tunapoandaa mkakati wa kutokomeza zao hili katika Wilaya za Tarime na Rorya na hali hii inaonyesha wanahusika moja kwa moja na biashara hii,” alisema.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum wilaya
ya Rorya kwa kutambua kuwa madawa ya kulevya ni kikwazo cha maendeleo ya
wananchi hasa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa, limekuwa likiendelea
kufanya operesheni katika maeneo yote yanayozunguka wilaya ili kutokomeza
madawa ya kulevya hasa bangi ambayo inalimwa katika maeneo mbalimbali wilayani
humo.
Hivyo kwa kushirikiana na wananchi
kupitia dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi jeshi hilo limeendelea
kupokea taarifa kutoka kwa wananchi na raia wema kuhusiana na uhalifu wa kilimo
cha bangi na wahalifu wenyewe wanaoendeleza kilimo hicho haramu ndani ya wilaya
ya Rorya.
Kutokana na taarifa hizo wameweza kugundua mashamba 22 ya bangi katika vijiji mbalimbali na hatimaye kuyateketeza na kuyafyekwa na kuyachoma moto.
Kutokana na taarifa hizo wameweza kugundua mashamba 22 ya bangi katika vijiji mbalimbali na hatimaye kuyateketeza na kuyafyekwa na kuyachoma moto.
Pia Jeshi hilo limefanikiwa
kukamata wahalifu wapatao sita waliojihusisha na kilimo hicho na kuwafikisha
mbele ya vyombo vyasheria ambako kesi mbalimbali zinaendelea mahakamani, na
baadhi ya bangi iliyokamatwa ndiyo hii inayoonekana katika picha mtandaoni hapa
ambayo rasmi imeteketezwa kwa kuchomwa moto na waandamizi wa mbio za mwenge wa
uhuru waliodhuru wilayani humo kukagua baadhi ya miradi ya maendeleo na kuweka
mawe ya msingi kwa baadhi ya miradi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)

0 Responses to “MWENGE WA UHURU WATEKETEZA SHAHENA YA BANGI WILAYANI RORYA MKOANI MARA.”
Post a Comment