Tuesday, September 2, 2014
PONDA AOMBA KESI YAKE ISIMAMISHWE
Do you like this story?
Dar es Salaam.
Wakili Nassoro Juma anayemtetea Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
Tanzania, Sheikh Issa Ponda ameiomba Mahakama Kuu itumie busara kusimamisha kesi
ya jinai inayomkabili mteja wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.
Ponda kupitia
wakili huyo, aliwasilisha maombi akitaka mahakama iamuru kesi hiyo inayomkabili
mkoani Morogoro isimame ili kusubiri kwanza uamuzi wa rufaa yake aliyokata
mahakamani hapo.
Katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Ponda anakabiliwa na mashtaka ya uchochezi
katika maeneo mbalimbali mkoani humo, likiwamo la kukaidi amri ya Mahakama ya
Kisutu.
Mahakama ya
Kisutu katika hukumu yake Mei 9, 2013, ilimtaka Sheikh Ponda awe mhubiri amani
katika jamii likiwa ni sharti la kifungo cha mwaka mmoja nje baada ya kumtia
hatiani katika kesi ya jinai mwaka 2012.
Katika kesi
hiyo, Ponda na wenzake walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kula njama, wizi wa
mali yenye thamani ya Sh59.6 milioni na kuingia kijinai kwa nia ya
kujimilikisha isivyo halali eneo la ardhi inayomilikiwa na Kampuni ya Agritanza
Ltd na uchochezi.
Hata hivyo,
Sheikh Ponda kupitia kwa mawakili wake alikata rufaa Mahakama Kuu kupinga
hukumu.
Kutokana na
rufaa hiyo, ndipo walipowasilisha maombi ya kusimamisha kesi hiyo katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.
Jaji Lawrence
Kaduri anayesikiliza maombi hayo alikubaliana na maombi ya Jamhuri na
kuahirisha shauri hilo hadi Septemba 10.
Via>Mwananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “PONDA AOMBA KESI YAKE ISIMAMISHWE”
Post a Comment