Tuesday, September 2, 2014
NDEGE YA KENYA YAANGUKA TANZANIA
Do you like this story?
Dar/Moro.
Ndege ya Kampuni ya Safari Express Limited imeanguka katika Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti na kuwateketeza watu watatu waliokuwamo ndani.
Ndege hiyo
yenye namba za usajili 5Y-SXP iliruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza Jumapili
saa 1:26 usiku ikielekea Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA) Kenya ambako
ilitakiwa kutua saa 2:36 usiku.
Meneja
Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Paschal Shelutete alikiri
ndege hiyo kuanguka kwenye hifadhi hiyo na walikuwa katika harakati za
kuitafuta.
Mkaguzi Mkuu
wa Ajali za Ndege nchini, kutoka Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, David
Nyamwihura alisema ajali hiyo ilitokea takriban maili 20 kutoka Serengeti,
katika eneo la Kogatembe na watu wote watatu waliokuwamo wamefariki dunia.
Meneja wa
Udhibiti wa JKIA, Clever Davor aliliambia gazeti la Daily Nation la Kenya kuwa
ndege hiyo ilipoteza mawasiliano na rada ya uwanja huo ikiwa imeruka angani urefu
wa futi 14,000.
Awali, Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege Kenya (KCAA) ilitoa taarifa juu ya kuchelewa kwa ndege
hiyo iliyokuwa ikitarajiwa kutua katika uwanja wa JKIA saa 2 usiku.
Jana asubuhi,
Kamanda wa Viwanja vya Ndege wa Kenya (KAPU), Joseph Ole Tito alithibitisha
kupotea kwa ndege hiyo kabla ya kuonekana baadaye katika Hifadhi ya Serengeti.
Polisi wa
Kenya hawakueleza ndege hiyo ya mizigo aina ya Fokker F-27-500 ilikuja nchini
kwa shughuli gani.
Ndege zote
zinazotoka Kenya kwenda nchi za jirani, huanzia safari zake katika viwanja vya
JKIA, Wilson au Wajir ili kuwa na usimamizi wa karibu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “NDEGE YA KENYA YAANGUKA TANZANIA”
Post a Comment