Friday, September 5, 2014
STARS YAIFUATA BURUNDI , 'ADEBAYOR', MORRIS, MANULA WATEMWA!
Do you like this story?
WANANDINGA 20 wa timu
ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wanaondoka leo alfajiri kwenda mjini
Bujumbura nchini Burundi tayari kwa mechi ya kimataifa ya Kirafiki dhidi ya
timu ya Taifa ya nchi hiyo itayochezwa septemba 7 mwaka huu (jumapili).
Mholanzi, Mart Nooij,
kocha mkuu wa Stars amewaambia waandishi wa habari kuwa amekiandaa vizuri
kikosi chake na kina matarajiao makubwa ya kulipa kisasi cha kufungwa mabao 3-0
na Burundi Aprili 26 mwaka huu katika mechi maalumu ya kuadhimisha miaka 50 ya
Muungano.
Katika mechi hiyo
iliyopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Stars iliyosheheni wachezaji
waliotoka katika mpango maalumu wa maboresho ya Taifa Stars uliofanywa na
shirikisho la soka Tanzania, TFF, ilishindwa kuhimili makali ya
washambuliaji wa Burundi kama vile Didier Kavumbagu na Amiss Tambwe.
“Natambua Burundi ina
wachezaji wazuri kama Tambwe, Kwizera na Kavumbagu, lakini kwa kikosi
tunachokwenda nacho tuna uhakika wa kufanya vizuri na kulipa kisasi kwani
Burundi walitufunga nyumbani.” Alisema Nooij.
Nooij alisema kuwa
wachezaji John Bocco, Aggrey Morris na Aishi Manula wameachwa katika msafara wa
Taifa Stars kutokana sababu mbalimbali.
Morris na Bocco ni
majeruhi wakati Manula ameachwa kwasababu tayari Nooij ana makipa wawili,
Mwadini Ali na Deogratius Munish ‘Dida’, hivyo hakuna sababu ya kwenda na kipa
huyo kinda.
Nooij aliwataja
wachezaji watakokweda Bujumburu kuwa ni makipa Mwadini Ali (Azam fc) na
Deogratius Munishi ‘Dida’, (Yanga).
Wachezaji wengine ni
Shomari Kapombe (Azam fc), Oscar Joshua (Yanga), Said Mourad (Azam fc), Nadir
Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Joram Mgeveke (Simba).
Wengine ni Saimon
Msuva (Yanga), Erasto Nyoni (Azam fc), Himid Mao (Azam fc), Amri Kiemba
(Simba), Haroun Chanongo (Simba), Salum Abubakary ‘Sure Boy’ (Azam fc), Mwinyi
Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Hamis Mcha ‘Vialli’ (Azam fc), Juma Luizio
(Zesco United, Zambia), Mrisho Ngasa (Yanga), Mbwana Samatta na Thomas
Ulimwengu (wote TP Mazembe, DR Congo).
.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “STARS YAIFUATA BURUNDI , 'ADEBAYOR', MORRIS, MANULA WATEMWA!”
Post a Comment