Friday, September 5, 2014
JIJI LA MBEYA KUPATIWA WATAALAM NA NHC.
Do you like this story?
![]() |
Meya wa jiji la Mbeya Bw Athanas kapunga akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari Ofisini kwake |
Shirika la nyumba la
Taifa NHC limekubali kutoa timu ya wataalam watakaosaidiana na Halmashauri ya
jiji la Mbeya katika suala zima la uchoraji mpya wa ramani
(MasterPlan) itakayotumika kwa ajili ya ujenzi wa makazi mapya katika
halmasahuri ya jiji la mbeya.
Kauli hiyo imetolewa
na Meya wa jiji la Mbeya Ndugu Athanas Kapunga mara baada ya kumalizika kwa
mazungumzo na wajumbe wa shirika hilo uliotembelea katika maeneo mbalimbali ya
miradi inayotalajiwa kutekelezwa na shirika hilo la NHC.
Kapunga amesema mara
baada ya kukutana na ujumbe huo ambao umeongozwa na Mkurugenzi wa shirika hilo
Ndugu Nehemia Mchechu umelidhia kupeleka timu hiyo ya wataalam ambayo
inashirikiana moja kwa moja na wataalam wa halmashauri hiyo ya jiji la Mbeya
katika kutengeneza mpango huo.
Aidha amesema timu
hiyo itaingia jijini humo mapema mwezi Octoba mwaka huu ili kuanza
mkakati huo kwa kuanza na hatua ya utoaji wa semina kwa wataalamu hao wa jiji
la mbeya hususani katika idara ya mipango miji.
Amesema maeneo ambayo
yatapewa kipaumbele katika utekelezaji wa shughuli hiyo ni pamoja na eneo la
Iwambi ambalo limegaiwa kwa wakazi wa jiji la Mbeya pamoja na eneo la stendi
kuu ya mabasi jijini humo.
Hata hivyo Ndugu
Athanas Kapunga ameweka wazi juu ya kuanza rasmi kwa ujenzi wa soko jipya la
kisasa katika eneo la Uhindini ambalo nalo ujenzi wake utakuwa chini ya shirika
hilo la nyumba NHC.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JIJI LA MBEYA KUPATIWA WATAALAM NA NHC.”
Post a Comment