Wednesday, October 15, 2014
MMILIKI WA FACEBOOK AMENUNUA HUU UPANDE WA KISIWA CHA HAWAII.
Do you like this story?
Kisiwa cha Hawaii |
Mark Zuckerberg na mke wake Priscilla Chan |
Mmiliki wa mtandao wa
kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg amenunua sehemu kubwa ya kisiwa cha Hawaii
iitwayo Kauai ambayo ni hekari 700 kwa dola za Kimarekani milioni 100 ambapo
atakuwa anamiliki eneo kubwa ambalo litaendana na hadhi ya bilionea, jarida la
Forbes limeripoti.
Hekari hizo 700
zitajumuisha beach resort, mashamba ya miwa na kilimo hai ambapo kwa sheria za
Hawaii beach resort hiyo lazima iachwe wazi kwa matumizi ya jamii kwa sababu
kisiwa hiko hakina sheria ya umiliki binafsi wa mchanga.
Zuckerberg
ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 30 anamiliki dola za Kimarekani billion
33 na anakua ni bilionea wa pili kununua sehemu ya Hawaii.
Mwaka jana
mwenyekiti wa Oracle Larry Ellison alinunua upande mzima wa Lanai, Hawaii kwa
dola milioni 600 ambapo stori nyingine zinasema Zuckerbug nae anaweza
akawa na nia ya kuanzisha majengo upande huo wa Lanai baada ya kuonekana na
mkewe Priscilla Chan kwenye maeneo hayo.
Haya
yatakua maendeleo mengine ya Zuckerberg kwani mwaka 2010 alikodisha jengo lake
ambalo lipo karibu na makao makuu ya office za Faceboook na mwaka
uliofata aliongeza makazi yenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 7 huko
Palo Alto, California, Marekani ambapo pia baada ya muda mfupi alitumia dola
milioni 30 kununua nyumba nne ambazo ziliunganishwa na makazi yake ya Palo
Alto.
Alivyoulizwa
kuhusu ripoti zilizotolewa hivi karibuni kuhusu matumizi yake ya pesa msemaji
wa Facebook alisema ‘Hatuna chochote cha kusema kuhusu maneno ambayo
hayana ukweli ila asante kwa kututafuta’
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MMILIKI WA FACEBOOK AMENUNUA HUU UPANDE WA KISIWA CHA HAWAII.”
Post a Comment