Thursday, October 9, 2014
WANAFUNZI WAONYWA KUACHA KUANGALIA PICHA ZA NGONO KWENYE MITANDAO.
Do you like this story?
WALIMU mkoani hapa
wametakiwa kushirikiana na wazazi katika kuwafundisha wanafunzi matumizi mazuri
ya mitandao hususan simu za mikononi katika mazingira yasiyoharibu maadili yao.
Akizungumza katika
mahafali ya kuhitimu darasa la saba katika shule ya Msingi Airport hivi
karibuni, Katibu wa Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani hapa,
Abdulikadri Mushi, alisema kuwa kwa sasa Dunia iko katika kipindi cha
utandawazi na watoto wadogo wako msitari wa mbele kuharibiwa na utandawazi huo,
kwani hutaka na wao kwenda na wakati.
Alisema kuwa, sasa
hivi watoto wadogo wanajua kutumia mitandao hasa simu za mikononi na kompyuta
na wengi hutumia kwa matumizi mabaya, ambayo husababisha kujifunza na kuiga
mambo mabaya.
“Utakuta watoto
wanaangalia picha chafu kwenye simu zao, pia hata kwenye kompyuta, kwani picha
hizo zinapatikana kwenye mtandao,” alisema Mushi.
Sambamba na hayo,
Mushi aliahidi kujenga jengo la choo ili kupunguza kero ya wanafunzi ya
kuhangaika baada ya kilichokuwepo awali shule hiyo kubomoka.
Naye Diwani wa Viti
Maalumu Kata ya Katubuka, Tatu Rajabu (CHADEMA), alisema jukumu la
kuhakikisha mtoto anakuwa katika mazingira mazuri yenye maadili ni la mzazi pia
walimu.
“Mzazi huachana na
mtoto asubuhi na mtoto hushinda na walimu kwa muda mwingi, hivyo walimu wawe na
mzigo katika kuwafundisha na kuwaonya watoto katika mambo ambayo hupelekea
kuharibika kwa maadili,” alisema Rajabu.
Kwa upande wa
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wanajeshi Wastaafu,
Nicas Bukobero, alisema kuwa kazi ya walimu ni kuwafundisha na kuwalea
wanafunzi katika maadili mema na sio kuwaacha waharibiwe na utandawazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANAFUNZI WAONYWA KUACHA KUANGALIA PICHA ZA NGONO KWENYE MITANDAO.”
Post a Comment