Wednesday, January 28, 2015
ANGALIA HII:MWANAFUNZI AJIFUNGUA NDANI YA DALADALA.
Do you like this story?
Mwanafunzi mmoja wa Shule ya Sekondari ya Keko amejifungua mtoto akiwa ndani ya daladala maeneo ya Mtoni Kwa Azizi Ally, jijini Dar es Salaam juzi tarehe 23.
Mwanafunzi huyo ambaye hakuweza
kupatikana jina lake mara moja, anasemekana alijifungua mtoto huyo bila ridhaa
yake wakati akiwa katika harakati za kuitoa mimba hiyo.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari,
msichana huyo anasemekana alikuwa amekunywa madawa makali kwa lengo la kuitoa
mimba hiyo ambayo anadaiwa kuificha hadi pale alipoumbuka mchana wa siku
hiyo.
Haikuweza kufahamika mara moja
alikopelekwa mtoto huyo baada ya tukio hilo wala hatua alizochukuliwa binti
huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ANGALIA HII:MWANAFUNZI AJIFUNGUA NDANI YA DALADALA.”
Post a Comment