Friday, January 9, 2015
OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAZUNGUMZIA MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WA MWEZI DESEMBA,2014
Do you like this story?
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo. |
Dotto
Mwaibale
MKURUGENZI wa
Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim
Kwesigabo alisema mfumuko wa bei wa taifa kutoka Januari hadi Desemba
mwaka jana umepungua hadi asilimia 6.1 kutoka wastani wa asilimia 7.9,
mwaka 2013.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Kwesigabo alisema kupungua kwa wastani huo kulichangiwa na
kupungua kwa kasi ya kupanda bei ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.
Alisema wastani
wa mfumuko wa bei ambao hujumuisha vyakula na nishati umepungua karibu nusu
mwaka 2014 kutoka asilimia 6.2 kwa mwaka 2013.
Pia alisema
kupungua kwa mfumuko wa bei wa mwaka 2104 kunamaanisha, kasi ya upandaji wa bei
za bidhaa na huduma kwa mwaka 2014 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo
mwaka 2013.
Kuhusu
mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Desemba 2014 umepungua hadi asilimia 4.8
kutoka asilimia 5.8 ilivyokuwa mwezi Novemba 2014. Hiyo ni kutokana na upandaji
wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha.
Kwa upande
wake Meneja Utafiti wa Biashara kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Johnson
Mnyella alisema moja kati ya malengo ya benki hiyo ni kuwa na mfumko wa bei
kati ya asilimia 5, hivyo wamefanikiwa kufikia pale wanapopataka.
Mnyella alisema
benki hiyo imekuwa ikiunga mkono jitihada mbalimbali pindi inapotokea mfumuko
wa bei na wamekuwa wakifanikiwa huku akisisitiza kuwa kutokana na kuwepo kwa
uzalishaji mkubwa wa chakula na mfumko wa bei utaendelea kuwa chini.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAZUNGUMZIA MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WA MWEZI DESEMBA,2014”
Post a Comment