Tuesday, January 13, 2015
UKOSEFU WA KAZI KWA VIJANA NI JANGA LA DUNIA.
Do you like this story?
Na Mwandishi Wetu
WIMBI kubwa la kuwa na vijana wasiokuwa na kazi limeelezwa kuwa tatizo
duniani kote na serikali mbalimbali zinatakiwa kuliangalia hilo kwa undani na
kulitatua. Kauli hiyo imetolewa na
Mratibu wa Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa shirika
la maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Mratibu huyo alisema hayo katika mazungumzo yake na Mkurugenzi Mtendaji
wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC) Abubakar Karsan. Alisema ukosefu wa kazi kwa sasa ni tatizo la
kijamii na kwamba, shauri hilo lisipoangaliwa kwa makini linaweza kuwa chanzo
cha matatizo makubwa ya usalama na amani katika taifa.
Alvaro Rodriguez ambaye alifika katika ofisi za UTPC kuangalia mambo
yanayofanyika katika ofisi hiyo wakati akiwa ziarani Mwanza wiki iliyopita,
alisema kama tatizo la ajira litaendelea kuwapo, vijana wanaoathirika wanaweza
kufikiria njia nyingine isiyo ya kistaarabu kufanikisha mambo yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UKOSEFU WA KAZI KWA VIJANA NI JANGA LA DUNIA.”
Post a Comment