Thursday, February 5, 2015
IVORY COAST YATINGA FAINALI AFCON 2015.
Do you like this story?
Timu ya Ivory Coast imefuzu kucheza fainali za Kombe
la Mataifa ya Afrika, AFCON, baada ya kuilaza Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
3-1 katika nusu fainali ya kwanza iliyochezwa Jumatano usiku katika mji wa
Bata.
Alikuwa
nahodha wa Ivory Coast Yaya Toure aliyeanza kuwanyanyua mashabiki wa Ivory
Coast alipofunga goli katika dakika ya 20 kutokana na mkwaju mkali na kumwaacha
mlinda mlago wa DR Congo, Kidiaba, asijue la kufanya.
DR
Congo wakasawazisha bao hilo katika dakika ya 24 kwa njia ya penalti likifungwa
na Mbokani Bezua.
Gervinho
akafunga bao la pili katika dakika ya 41. Hivyo hadi mapumziko Ivory Coast
ilikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Kipindi
cha pili timu hizo ziliendelea kushambuliana. Wilfried Kanon alikamilisha
sherehe kwa timu yake ya Ivory Coast alipofunga bao la tatu katika dakika ya
68. Kwa matokeo hayo Ivory Coast imetinga fainali za michuano ya Afcon mwaka
2015, ambapo inamsubiri mshindi wa nusu fainali ya pili, kati ya Ghana na
wenyeji Equatorial Guinea, Alhamisi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “IVORY COAST YATINGA FAINALI AFCON 2015.”
Post a Comment