Tuesday, February 3, 2015
MBIO ZA KILIMANJARO MARATHON ZAZINDULIWA RASMI MKOANI KILIMANJARO MJINI MOSHI.
Do you like this story?
KILIMANJARO
Mashindano ya 13 kimataifa ya riadha ya Kilimanjaro marathoni
mwaka 2015 ya mezinduliwa rasmi mkoani Kilimanjaro ambapo Tanzania
imetamba kuwa itag’ara katika mashindano hayo yanayo tarajiwa
kufanyika mwezi machi mwaka huu mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza
kwa niaba ya raisi wa chama cha riadha nchini kwenye uzinduzi wa
mashindano hayo uliyofanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, mwenyekiti wa
chama cha riadha mkoani Kilimanjaro Listone Metacha alisema Tanzania imewaanda
vilivyo wachezaji wake mapema badala ya kukurupuka katika dakika za
mwisho.
Akizindua mbio
hizo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro leonidas Gama, katibu
tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Severin Kaitwa, amewataka watanzania
kujitokeza kwa wingi katika kushiriki mashindano hayo, ambayo mbali na
kuchangia uchumi wa nchi ya Tanzania, pia yanaipa sifa kubwa kimataifa.
Meneja wa bia
ya Kilimanjaro ambayo ni mdhamini mkuu wa mashindano hayo Pamela Kikuli,
alisema kwa miaka 13 sasa wamekuwa wakidhamini mashindano hayo, ambapo mwaka
huu wametenga kiasi cha shilingi milioni 20, kwa washindi 10 wa
mbio ndefu za kilometa 42, ambapo washindi wa kike na wa kiume kwa mshindi wa
kwanza atajinyakulia kitita cha shilingi milioni nne na mshindi wa pili
atanyakua shilingi milioni mbili huku mshindi watatu kwa upande wa wanaume na
wanawake wataondoka na shilingi milioni moja kila mmoja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MBIO ZA KILIMANJARO MARATHON ZAZINDULIWA RASMI MKOANI KILIMANJARO MJINI MOSHI.”
Post a Comment