Wednesday, February 4, 2015
NDEGE YA TAIWAN YAANGUKA MTONI NA KUUA WATU 12.
Do you like this story?
![]() |
| Waokoaji wakinasua watu waliokuwa ndani ya ndege hiyo. |
Ndege inayoimilikiwa na Shirika la Ndege la Taiwan, la TransAsia imepata
ajali na kuangukia kwenye mto katika mji mkuu, Taipei na kuua watu 12.
Vyombo vya habari vya Taiwan vimesema watu zaidi ya 50 walikuwa ndani ya
ndege hiyo, wakati ajali ilipotokea na idadi kubwa ya watu wameripotiwa
kujeruhiwa.
Shirika la Habari la Taiwan limeonesha picha ya ndege hiyo ikiwa imezama
kwa kiasi kikubwa katika mto Keelung.
Chanzo cha ajali bado hakijajulikana.
Watu kadhaa wameokolewa na kupelekwa hospitali na wengine 10 bado
wamenasa katika ndege hiyo.
Ndege hiyo ilikuwa ikiruka kutoka uwanja wa ndege wa
Songdshan Taipei kuelekea uwanja wa ndege wa Kinmen nje ya Taiwan.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)



0 Responses to “NDEGE YA TAIWAN YAANGUKA MTONI NA KUUA WATU 12. ”
Post a Comment