Wednesday, February 4, 2015
WIZARA YAWATAKA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI KUWAKATIA BIMA WAFANYAKAZI WAO
Do you like this story?
![]() |
| Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia akijibu swali Bungeni mjini Dodoma. |
Na
Lorietha Laurence-Maelezo Dodoma.
Naibu
Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia amewataka wamiliki
wa vyombo vya habari kuwakatia wafanyakazi wao bima ili ziweze kuwasaidia
wakati wanapopatwa na madhara wakiza kazini.
Akijibu
swali la mbunge wa viti maalum Anna Mallac, kuhusu
mpango wa Serikali kuwapatia ulinzi waandishi pale wanapokuwa wakifanya kazi
katika matukio hatari, Naibu Waziri Nkamia
alisema kuwa serikali inafahamu mazingira ya kazi ya wanahabari na
inawajibika kikatiba katika kutoa ulinzi kwa raia wake wote wakiwemo
wanahabari.
“Uandishi
wa habari ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine
muhimu katika jamii kama ilivyo taaluma ya sheria ualimu na udakatari na ni
muhimu kufahamu na kuzingatia miiko ya taaluma pale wanapokuwa
katika eneo la kazi”alisema Nkamia.
Aidha
alibainisha kuwa jukumu la kwanza kwa waandishi wa habari ni
kujilinda na kujihami wao wenyewe kwa kuwa wanayafahamu mazingira yao ya kazi
na pia kuzingatia miiko ya taaluma yao kwa kuangalia wanayotakiwa
kufanya na kutofanya katika eneo husika. Aliongeza
kuwa wanahabari wanatakiwa wazingatie sheria bila shuruti kwa kuwa nao ni
wananchi kama walivyo wananchi wengine na hakuna aliye juu ya sheria .
Hata
hivyo Serikali imekuwa ikiwapatia waandishi wa habari vifaa maalum
katika matukio mbalimbali ya kitaifa ikiwemo
vitambulisho na mavazi maaalum ya kuwatambulisha wakiwa katika eneo la kazi
ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuwalinda na madhara yeyote.
Naibu
Waziri Nkamia alieleza kuwa kwa sasa wizara yake imekuwa ikiandaa muswada wa
sheria ya vyombo vya habari ambao utawasilishwa mbugeni wakati wowote kuanza
sasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “WIZARA YAWATAKA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI KUWAKATIA BIMA WAFANYAKAZI WAO ”
Post a Comment