Tuesday, February 3, 2015
WAZIRI WA UJENZI DKT. MAGUFULI AKAGUA BARABARA MKOANI MBEYA NA RUKWA.
Do you like this story?
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli |
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia wakazi wa mji
wa Tunduma mkoani Mbeya kuwa Serikali itajenga barabara ya njia nne katika mji
huo ili kupunguza msongamano wa magari na kuuwezesha mji huo kuwa wa kisasa na
kibiashara.
Amesema hayo katika ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya barabara
inayoendelea katika mikoa ya Mbeya na Rukwa ambapo akiwa mjini Tunduma
amekutana na wananchi wanaofanyabiashara katika mji huo.
“Dumisheni umoja,amani na mshikamano ili mfanye biashara zenu na kukuza
uchumi nasi tutahakikisha tunajenga barabara ya njia nne ili kupunguza
msongamano wa magari na kuuwezesha mji wa Tunduma kuwa wa kisasa na kibiashara
na hivyo kuwa mahali pazuri pa watu kuishi”,amefafanua waziri Magufuli.
Katika ziara hiyo waziri Magufuli amekagua mizani ya Nkangamo na barabara
ya Tunduma –Sumbawanga KM 225, iliyojengwa kwa kiwango cha lami na kuwataka
wananchi wa mkoa wa Rukwa kutumia barabara hiyo kukuza uchumi wao na wa mkoa
wao kwa kufanyakazi kwa bidii.
Akihutunbia wananchi wa Sumbawanga Waziri Dkt. Magufuli amewataka
wananchi kutambua kuwa barabara za lami zinajengwa kwa gharama kubwa hivyo
wazitumie kwa manufaa na wale walioko kwenye hifadhi ya barabara wabomoe nyumba
zao mapema ili kuwezesha ujenzi kufanyika kwa wakati.
Waziri Magufuli amesema Serikali iko katika hatua za awali kujenga
barabara ya Matai-Kasesha KM 50 kwa kiwango cha lami ili kuunganisha mkoa wa
Rukwa nan chi ya Zambia na hivyo kuvutia wawekezaji wengi kuwekeza mjini
Sumbawanga na hivyo kutoa fursa za ajira na uchumi kwa wananchi.
Waziri Magufuli yuko katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya barabara katika
mikoa ya Mbeya,Rukwa,Katavi na Tabora ambako kuna miradi mikubwa ya ujenzi wa
barabara za lami inayoendelea.
Imetayarishwa na kitSengo cha habari na mawasiliano serikalini wizara ya
ujenzi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAZIRI WA UJENZI DKT. MAGUFULI AKAGUA BARABARA MKOANI MBEYA NA RUKWA.”
Post a Comment