Sunday, March 22, 2015

MAMLAKA YA MAJI SAFI JIJINI MBEYA ( UWSA)YATAKIWA KUONGEZA UZALISHAJI WA MAJI.


Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya wiki ya maji 2015 katika viwanja vya Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Mbeya (UWSA)



Watumishi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Mbeya (UWSA)



Jjaji Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya ambaye pia ni Mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Mbeya(UWSA)  Atuganile Ngwala akizungumza katika maadhimisho hayo.






Afisa Afya na usafishaji jiji la Mbeya Ndugu Odas Aron akitoa maada katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji



Burudani






Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akipokea msaada wa vifaa kutoka kwa mamlaka hiyo kwa ajili ya kusaidia vikundi vya Ulinzi shirikishi katika maeneo ya Vyanzo vya maji ambavyo ni Makoti ya kuzuia Mvua,Viatu maalum pamoja na Tochi.




Na Mwandishi wetu,Mbeya
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mbeya (Uwsa) imetakiwa kuongeza uzalisha wa maji safi na salama    kutoka  asilimia 96 hadi asilimia 110 kwa masaa 15 na 24.


Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa kwenye kilele cha Maadhimisho ya wiki ya maji Duniani  mwaka huu katika viwanja vya mamlaka hiyo.


Amesema pamoja na mamlaka hiyo kuzalisha maji safi na salama na kuyasambaza kwa wakazi wake wa jiji la Mbeya  kwa asilimia 96 nivema uzalishaji huo ukapanda walau kufikia asalimia 110 ili kukidhi haja ya wateja wake ambao kila siku  huongezeka.


Amesema kutokana na jiji la mbeya kupanuka kumechangia kwa kiwango kikubwa kuongezeka kwa wateja wapya hivyo umefika wakati kwa mamlaka hiyo kuangalia upya uwezekano wa kuongeza uzaishaji wake.


Aidha Mkuu huyo wa wilaya ameiagiza Mamlaka hiyo kuhakikisha inaboresha miundombinu ya maji safi na maji taka.


Pia Nyirembe ametoa wito kwa Mamlaka hiyo kuhakikisha inapima maeneo yote ya vyanzo vya maji pamoja na kuwa na hati miliki za maeneo hayo ili kuweza kupitisha sheria mpya itakayo wabana waharibu na wavamizi wa vyanzo vya maji katika maeneo hayo.


Awali akisaoma lisala kwa niaba ya wafanya kazi wa Mamlaka hiyo Ndugu Amiry Sapi fundi Mkuu wa Malaka hiyo amesema katika kuadhimisha siku hiyo mamlaka hiyo kwa kushirikiana na ofisi za bonde la ziwa rukwa wameweza kutoa elimu kwa wateja kuhusu huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo.


Pia amesema mahitaji ya maji katika jiji la mbeya ni mita za ujazo 38,000 kwa siku ambapo mahitaji hayo hupanda wakati wa kiangazi kufikia mita za ujazo 43,000 kwa miezi ya Septemba hadi Novemba.

Mwisho.



0 Responses to “ MAMLAKA YA MAJI SAFI JIJINI MBEYA ( UWSA)YATAKIWA KUONGEZA UZALISHAJI WA MAJI.”

Post a Comment

More to Read