Saturday, April 4, 2015

SIMBA WAFURA HASIRA MECHI KUAHIRISHWA SHINYANGA, KAGERA RAHA TU!






KUFUATIA mvua zinazoendelea kunyesha Mjini Shinyanga, mechi ya ligi kuu baina ya Kagera Sugar dhidi ya Simba iliyotakiwa kupigwa leo jioni majira ya saa 10:30 imeahirishwa kutokana na uwanja kujaa maji.
Uongozi wa Simba umechukizwa na kuahirishwa kwa mechi hiyo ukidai kuwa wanalazimika kuingia gharama kubwa ya kuendelea kukaa Shinyanga bila sababu.

Afisa habari wa Simba, Hajji Sunday Manara amesema kuwa uwanja ulikuwa katika hali ya kuchezeka, lakini ameshangazwa na uamuzi wa kuahirisha mechi.

"Kulikuwa na maji magoli yote mawili, sehemu ya kuchezea ilikuwa sawa,  tukasema tununue magodoro ya kufyonza maji kwa gharama zetu, lakini wamegoma. Nadhani wameahirisha kwasababu ya maslahi. Wao wanataka mapato, lakini hawaangalii upande mwingine. Tunakaaje hapa Shinyanga, gharama hizi anaendelea kulipa nani, mpira wa nchi hii hautaendelea kamwe!" Amesema Hajji.

Wachezaji wa Simba walionekana kuwa tayari kucheza mechi hiyo.
"Sisi tuko poa tu, kama vipi tucheze tu". Amesema Jonas Mkude.
Hata hivyo uwanja wa Kambarage haukuwa katika hali ya kuchezewa mechi, sema Simba wanataka kukwepa gharama za kambi.
Kwa upande wa Kagera Sugar, Mratibu wa timu hiyo, Mohammed Hussein ameridhishwa na maamuzi ya kuahirishwa mechi.

"Muamuzi ndiye aliyefanya maamuzi, lakini watu wanajadili suala la mapato kwasababu watu hawajajitokeza wengi, kama ni hivyo hata mimi nakubali". Amesema Mohamed.


0 Responses to “SIMBA WAFURA HASIRA MECHI KUAHIRISHWA SHINYANGA, KAGERA RAHA TU!”

Post a Comment

More to Read