Saturday, April 4, 2015

MTANZANIA ANASWA KATIKA SHAMBULIO LA KIGAIDI GARASSA UNIVERSITY.


Kenya Mtanzania mmoja ambaye hajafahamika amekamatwa kuhusiana na shambulio la kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa, Kenya.

Taarifa zilizopatikana jana usiku na kutangazwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), zilieleza kuwa Mtanzania huyo anahojiwa kuwapo kwake katika eneo hilo hasa ikizingatiwa kwamba siyo mwanafunzi wala mtumishi katika chuo hicho.

Taarifa hizo zinasema kuwa Mtanzania huyo ni miongoni mwa watu wanne waliokuwa wamejificha na katika mabweni ya chuo hicho na kati yao, wawili walibainika kuwa ni wanafunzi.

Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba alipoulizwa jana kuhusu Mtanzania huyo, alisema atatoa taarifa rasmi kwa taratibu za jeshi hilo.


0 Responses to “MTANZANIA ANASWA KATIKA SHAMBULIO LA KIGAIDI GARASSA UNIVERSITY.”

Post a Comment

More to Read