Saturday, April 4, 2015

FoS WAWALILIA SIMBA UKAWA





'Mashabiki saba wa Simba SC walifariki kwa ajali ya gari jana mkoani Morogoro wakiwa safarini kwenda mjini Shinyanga kuisapoti timu yao dhidi ya Kagera Sugar FC.'
KUNDI la Marafiki wa Simba SC (Friends of Simba - FoS), leo limetuma salamu za rambirambi kwa tawi la Mpira na Maendeleo kutokana na vifo vya mashabiki wa Simba SC wa kundi hilo jana.

Mashabiki saba wa Simba SC kutoka kundi la Mpira na Maendeleo maarufu Simba Ukawa walifariki kwa ajali ya gari jana mkoani Morogoro huku wengine zaidi ya 10 wakijeruhiwa.

Mwenyekiti wa FoS, Zacharia Hanspope, ameuambia mtandao huu kuwa wamezipokea kwa masikitiko taarifa za tukio hilo na kwamba kundi lake litatoa rambirambi ya Sh. milioni mbili kwa familia za marehemu.

0 Responses to “FoS WAWALILIA SIMBA UKAWA”

Post a Comment

More to Read