Saturday, April 4, 2015

UHURU KENYATTA ATANGAZA SIKU 3 ZA MAOMBOLEZO BAADA YA JANGA LA GARISSA UNIVERSITY




Rais uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza maombolezo ya sikutatu kitaifa wakati akilihutubia taifa hilo kufuatia shambulio la kikundi cha al-Shabaab kwenye Chuo Kikuu cha Garisa Alhamisi iliyopita ambapo watu wapatao 150 waliuawa.

Kabla ya Rais kenyata kutangaza siku tatu za maombolezo Utawala wa Kenya umesema kuwa watu watano wametiwa nguvuni kufuatia shambulio hilo ambapo taarifa za hivi karibuni kutoka chuoni hapo zinasema mwanafunzi mmoja wa kike amepatikana akiwa amejificha chini ya godoro na kuokolewa saa tano asubuhi leo na maafisa wa chama cha msalaba mwekundu.

Serikali ya Kenya tayari imekifunga chuo hicho na kufuatia kufungwa wake wanafunzi wake walikuwa wanatarajiwa kurejeshwa chuoni hapo leo ili kuchukua vitu vyao kabla ya kurejeshwa makwao.

0 Responses to “UHURU KENYATTA ATANGAZA SIKU 3 ZA MAOMBOLEZO BAADA YA JANGA LA GARISSA UNIVERSITY”

Post a Comment

More to Read