Monday, April 13, 2015

MWINGINE HUYU HAPA KAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUTUMIA VIBAYA MITANDAO YA KIJAMII




Kijana mmoja Robert Mungai yeye tayari yuko mikononi mwa Mahakama, kinachosubiriwa ni Mahakama kuendelea kusikiliza kesi yake na kuamua hukumu pia kutokana na jamaa huyo kukabiliwa na kesi ya kuandika ujumbe wa uongo kwenye ukurasa wake wa Facebook siku ya April 4 2015.

Polisi Kenya wamesema Robert aliandika ujumbe wa kuwaonya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Egerton University kilichoko Njoro, ambapo ujumbe alioandika alikuwa akiwataarifu wenzake kuwa Kikundi cha Al-Shabaab kitashambulia.Robert alikataa kutenda kosa hilo lakini Polisi walikataa asiachiliwe kwa dhamana kwa kuwa uchunguzi bado haujakamilika.

Imeripotiwa na vyombo vya habari Kenya, wanasema kwa Sheria ya nchi hiyo ilivyo huenda hukumu yake ikawa kifungo cha zaidi ya miaka ishirini.

Alan Wadi Okengo aliwahi kuingia kwenye HEADLINES pia toka Kenya January 2015 baada ya kuhukumiwa mwaka mmoja jela na kulipa faini kwa kosa la kumtukana RaisKenyatta mtandaoni.

0 Responses to “ MWINGINE HUYU HAPA KAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUTUMIA VIBAYA MITANDAO YA KIJAMII ”

Post a Comment

More to Read