Friday, April 10, 2015
FIFA YATOA VIWANGO VIPYA VYA SOKA.
Do you like this story?
Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) limetoa viwango
vipya vya soka duniani huku Tanzania na Rwanda zikishuka kwa nchi za Afrika ya
Mashariki wakati Kenya, Uganda na Burundi zikipanda viwango.
Kushuka na kupanda kwa viwango kunatokana na mechi za
kirafiki za kimataifa za Fifa zilizofanyika mwezi Machi , ambazo matokeo yake
ni sehemu ya kigezo.
Tanzania, baada ya kutoka droo ya 1-1 na timu ya Malawi
katika moja ya mechi hizo za kirafiki, imeshuka kutoka nafasi ya 100 mpaka ya
107 huku Rwanda ikishuka nafasi 10 hadi ya 74 baada ya kupokea kichapo kutoka
kwa Zambia cha magoli 2-0 mwezi Machi.
Uganda ndio nchi inayoongoza katika Afrika ya Mashariki
ikipanda nafasi mbili juu na kushika nafasi ya 72 baada ya kuwafunga Nigeria
1-0.
Burundi nayo imepanda kutoka nafasi ya 126 mpaka ya 123
mbali ya kutoka droo ya 2-2 na timu ya Mauritius.
Kenya pia imepanda nafasi moja juu na sasa ipo ya 117 huku
ikiwa na rekodi ya kuifunga Shelisheli 2-0 katika mechi yake ya kirafiki.
Mbali na Afrika ya Mashariki, kiujumla kumekuwa na
mabadiliko makubwa katika viwango hivyo vya mwezi April.
Miongoni mwa nchi zilizopanda ni Belgium ikiwa ya tatu baada
ya kupanda juu nafasi moja kufuatia ushindi wake katika michuano ya Ulaya ya
EUFA.
Brazil pia ni miongoni mwa nchi zilizopanda, ikiwa ya ya 5,
ikipanda nafasi 1.
Nchi 10 bora katika viwango vya fifa ni
1. Ujerumani
2. Argentina
3. Belgium
4. Colombia
5. Brazil
6. Netherlands
7. Portugal
8. Uruguay
9. Swizerland
10. Uhispania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “FIFA YATOA VIWANGO VIPYA VYA SOKA.”
Post a Comment