Tuesday, April 14, 2015

AKUTWA NA FUVU LA KICHWA CHA BINADAMU.




Na Agness Munubi_katavi
JESHI la Polisi Mkoani Katavi linamshikilia Mganga  mmoja wa jadi  mkazi wa kijiji cha kakese mbugani wilayani mpanda baada ya kukutwa na  fuvu la kichwa cha binadamu  pamoja na nyara za Serikali.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani  Katavi  SACP Dhahiri Kidavashari amethitisha kukamatwa kwa mganga huyo na kumtaja kuwa ni Kabichi Nhulu ambaye alilihifadhi fuvu hilo ndani ya choo ikiwa analitumia katika  kuimarisha uganga wake ambapo wagonjwa wakienda kwake ukalia fuvu hilo.

Sauti ya katavi imemtaka Kamanda huyo kutoa ufafanuzi juu ya sheria ya waganga wa jadi ikiwa amefafanua kuwa mganga wa jadi anatakiwa kuwa na kibali na  hata kama ana kibali kukutwa na kiungo cha binadamu ama nyara za serikali ni kosa kisheria.
 
Aidha  Kidavashari amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika mapambano dhidi ya uhalifu mkoani hapa kwani tarifa za mganga huyo zilitolewa na raia wema.

0 Responses to “AKUTWA NA FUVU LA KICHWA CHA BINADAMU. ”

Post a Comment

More to Read