Tuesday, April 14, 2015
SOMALIA: AL SHABAAB YASHAMBULIA NA KUUA WATU 9 MOGADISHU.
Do you like this story?
Watu 9 wameripotiwa
kuuawa katika jengo ya Wizara ya Elimu mjini Mogadishu, Somalia. Vyombo vya
habari mjini Mogadishu vimeripoti kuwa wavamizi hao walilipua bomu lililotegwa
ndani ya gari kwenye ukuta wa jengo la waizara ya elimu nchini humo.
Kabla ya wavamizi kadhaa kuingia ndani ya
jengo walianza kwa kupiga risasi za kutishia, kisha kulipua bomu na
risasi ziliendelea kusikisa ndani ya jengo hilo wakati Al Shabaab wakitekeleza
unyama huo wa kutisha.
Msemaji wa wa kitengo cha mashambulizi cha kundi
la wapiganaji wa Al Shabaab Sheikh Abdiasis Abu Musab, amethibitisha kuwa ni
wao waliotekeleza shambulizi hilo na kuwa ''wapiganaji wetu wamekwisha ingia
ndani ya jengo hilo la wizara ya elimu''.
Kutokana na ripoti ya Polisi mjini Mogadishu
inasema, mapigano yanaendelea hadi sasa ndani ya jengo hilo baina ya majeshi ya
serikali na wapiganaji.
Wapiganaji wa Al Shabaab wametekeleza
mashambulizi kama haya katika siku za hivi punde katika Chuo Kikuu cha Garissa
mjini Nairobi nchini Kenya na kuuwa watu wapatao 150 huku wakiacha mamia ya
majeruhi wakiendelea kuugulia wakati huo wapiganaji wote watano wa al shaabab
wakiuawa na jeshi la serikali nchini Kenya.
Mwezi uliopita wapiganaji wa Al Shabaab
walishambulia hoteli moja mjini Mogadishu uvamizi huo ulikamilika siku mbili
zilizofwatia.
Waandishi wa habari walioshuhudia matukio
kabla ya uvamizi huo wanadai kuwa kulikuwa na milipuko miwili mikubwa kabla ya
milio ya risasi kuanza kusikika kutoka jengo hilo. Hakuna kundi
lililothibitisha kutekeleza shambulizi hilo lakini Al Shabaab imekuwa ikitumia
mbinu kama zilizotumika leo.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, kundi hilo la
waislamu la Al Shabaab linapinga serikali iliyoko sasa ambayo inaungwa mkono na
majeshi ya Umoja wa Afrika.
CHANZO NA BBC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SOMALIA: AL SHABAAB YASHAMBULIA NA KUUA WATU 9 MOGADISHU.”
Post a Comment