Monday, April 6, 2015

KUNDI LA NYUKI LASABABISHA MAUAJI HUKO GEITA




Familia ya Diwani wa viti Maalum Mkoa wa Geita, Helena Mahona imevamiwa na kushambuliwa na nyuki ambao wamejeruhi mama mmoja na watoto wawili na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye ni shangazi wa Diwani huyo.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Joseph Majebele amesema alikuwa mbali na eneo hilo lakini akapewa taarifa ya kutokea kwa tukio hilo kwa njia ya simu na watu walioshuhudia.

Kamanda wa Polisi Geita, Peter Kakamba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa marehemu alifariki hapo hapo kwenye tukio huku majeruhi wakikimbizwa Hospitai na hali zao zinaendelea vizuri.

0 Responses to “KUNDI LA NYUKI LASABABISHA MAUAJI HUKO GEITA”

Post a Comment

More to Read