Monday, April 6, 2015

MLEMAVU AAMUA KUISHI DARINI KWA MIEZI MINNE MFULULIZO KUKWEPA MAFURIKO HUKO MTWARA




Mtoto Abdul Mohamedi ambaye ni mlemavu wa viungo, amelazimika kuishi darini kwa miezi minne mfululizo kukwepa kudhuriwa na mafuriko kutokana  mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mtwara.

Bibi wa mtoto huyo Zainabu Lipuga alisema jana kuwa alimpandisha darini mjukuu wake Novemba mwaka jana baada ya mafuriko yaliyotekea kipindi hicho.

Nilipoona mvua zinanyesha nikaona bora nimnusuru mjukuu wangu asisombwe na mafuriko kwa vile sina nguvu za kuweza kumpandisha na kumteremsha mara kwa mara,” alisema Lipuga
Bibi huyo amesema baba wa mtoto hajulikani alipo na jukumu la kumlea limeachwa mikononi mwake bila msaada.

Zaidi ya nyumba 200 zilizingirwa na maji kutokana na mvua kusababisha hasara kwa wananchi ikiwemo kuharibika mali zao zikiwamo nguo na vyakula.

0 Responses to “MLEMAVU AAMUA KUISHI DARINI KWA MIEZI MINNE MFULULIZO KUKWEPA MAFURIKO HUKO MTWARA ”

Post a Comment

More to Read