Monday, April 6, 2015

KIJANA AFIKA OFISI ZA RADIO FREE KUOMBA MSAADA,TAFADHALI MSAADA WAKO UNATAKIWA.




Kushoto ni uso, upande wa juu kulia ni mkono na chini kulia ni mguu

Ni kijana mtanzania ambaye nae alikuwa na ndoto zake lakini kwa hali aliyonayo sio rahisi kuzitimiza.

Alikuja ofisini hivi karibuni apate msaada wa kutangazwa ili watu wamsaidie aweze kupata matibabu.

Kwa ujumla maisha yake ni magumu sana kutokana na kunyanya paliwa na jamii kwa kiasi kikubwa,vyombo vya usafiri havikubali kumbeba hivyo mara nyingi hulazimika kutembea kwa miguu kama hana pesa ya kupanda pikipiki.

Kwa hakika anahitaji msaada sana,hawezi kufanya kazi labda atapata pesa kidogo,jamii inamnyanyapaa lakini ana haki ya kuendelea kuishi.

Huenda usiwe na uwezo wa pesa za kutosha kupata  matibabu lakini kidogo utakacho msaidia kinaweza kumwezesha kula,na kupata hata mahitaji ya muhimu ya kibinadamu au wewe ukimpa kidogo na mwingine akimpa kidogo akiunganisha atapata kikubwa.

Tafadhali usisite kumsaidia na hii ndiyo namba yake 0755 860 561kumbuka anahitaji faraja sana kwahyo usimsumbue kubeep na maudhi mengine.

0 Responses to “KIJANA AFIKA OFISI ZA RADIO FREE KUOMBA MSAADA,TAFADHALI MSAADA WAKO UNATAKIWA.”

Post a Comment

More to Read