Friday, April 10, 2015

LIGI KUU YA VODACOM KUENDELEA WIKIENDI HII YANGA KUVAANA NA MBEYA CITY.






Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inatarajiwa kuendelea wikiendi hii
katika viwanja sita tofauti nchini, viwanja vinne vikitimua vumbi kesho jumamosi,
na michezo miwili kuchezwa siku ya jumapili.

Jumamosi JKT Ruvu watakua wenyeji wa Coastal Union katika Uwanja
wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es salaam, huku wakata miwa wa Kagera
Sugar wakiwakaribisha maafande wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Kambarage
mjini Shinyanga.

Timu ya Mtibwa Sugar watawakaribisha Azam FC kwenye uwanja wa
Manungu-Turiani mjini Morogoro,nayo
Ndanda FC watakua wenyeji wa timu ya Tanzania Prisons mjini Mtwara
katika uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Ligi hiyo itaendelea siku ya jumapili katika uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam, Young Africans watawakaribisha timu ya Mbeya City kutoka
mkoani Mbeya, huku mjini Shinyanga katika uwanja wa Kambarage wenyeji timu ya
Stand United wakiwakaribisha maafande wa
timu ya Polisi Morogoro.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

0 Responses to “LIGI KUU YA VODACOM KUENDELEA WIKIENDI HII YANGA KUVAANA NA MBEYA CITY.”

Post a Comment

More to Read