Wednesday, April 8, 2015
TFF YAMPONGEZA TENGA.
Do you like this story?
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF Jamal Malinzi, amempongeza Bw
Leodgar Tenga kwa kuchaguliwa kuendelea kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).
Aidha
Rais Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa wajumbe waliochaguliwa kuwa
wajumbe wapya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu baranai Afrika (CAF) na
Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA.
Katika
salamu hizo na nakala zake kutumwa kwa Rais wa CAF Bw. Issa Haytou na Rais wa
FIFA Bw. Blatter, Malinzi amewatakia kila la kheri katika majukumu hayo
mapya,na kwa ajili ya maendeleo ya mpira wa miguu duniani.
Tenga
amechaguliwa nafasi hiyo baada ya kuwa mgombea pekee kutoka kanda ya Afrika
Mashariki aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo na kuungwa mkono na nchi zote
wanachama wa CECAFA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TFF YAMPONGEZA TENGA.”
Post a Comment