Wednesday, April 8, 2015

DIAMOND PLATINUMZ ATAJWA KUWANIA TUZO YA 'RADIO AFRO AUSTRALIA SONG OF THE YEAR 2014’





Muonekano wa kipengele cha tuzo anachowania Diamond Platinumz.
STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' ametajwa kuwania tuzo ya 'Radio AFRO Australia Song of the Year 2014' kupitia wimbo wake wa Number 1 Remix’ aliyomshirikisha staa wa Nigeria Davido.

Wasanii wengine kutoka Afrika wanaowania Tuzo hizo ni pamoja na Davido ambaye ana nyimbo nne zilizoingia, Bebe Cool ana nyimbo mbili, P-Square wana nyimbo nne, 2Face, AKA, Cassper Nyovest na Iyanya. 

Tuzo hizi hufanyika kila mwaka na wasikilizaji wa Afro Radio ya Australia hupiga kura mtandanoni na msanii atakayepata kura nyingi ndiye anaibuka mshindi.
Kumpigia kura Diamond na kumfanya ashinde bonyeza hapa.

0 Responses to “DIAMOND PLATINUMZ ATAJWA KUWANIA TUZO YA 'RADIO AFRO AUSTRALIA SONG OF THE YEAR 2014’”

Post a Comment

More to Read